Mabingwa watetezi, Yanga SC |
Na Prince Akbar
KLABU za AS Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
(DRC) na URA ya Uganda zinatarajia kuwasili nchini Julai 12 mwaka huu kushiriki
michuano ya Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame)
itakayofanyika Dar es Salaam kuanzia Julai 14 mwaka huu.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace
Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba AS Vita Club
ambayo iko kundi A pamoja na timu za Simba (Tanzania Bara), Ports (Djibouti) na
URA itawasili saa 1.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways ikipitia Nairobi.
Nayo URA itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA) jioni ya siku hiyo kwa ndege ya Air Uganda. AS Vita imepangiwa
kufikia hoteli ya Rombo Green View wakati URA itakuwa hoteli ya Royal
Valentino.
Katika michuano hiyo, mabingwa watetezi Yanga watafungua
dimba na Atletico ya Burundi katika mchezo wa Kundi C Julai 14, mwaka huu Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam, wakati wapinzani wao wa jadi, Simba SC waliowekwa
Kundi A, wataanza na URA ya Uganda Julai 16, kwenye Uwanja huo huo.
Wawakilishi wengine wa Tanzania katika michuano hiyo, Azam
FC wao wataanza na Mafunzo ya Zanzibar katika mchezo wa Kundi B, Uwanja wa
Chamazi, Julai 15.
0 comments:
Post a Comment