|
MANENO TOFAUTI: Mama yake Mario Balotelli, Rose Barwuah anaingiza pauni 6 kwa saa
ANAPATA mshahara wa pauni 120,000 kwa wiki, anapenda kunywa shampeni ya Vintage kwa kupiga tarumbeta na mamia ya pauni anatoa sadaka kanisani.
Lakini inaonekana kama Mario Balotelli hana msaada kwa mama yake, ambaye anafanya kazi 'ya kufanya usafi' katika ofisi, iliyo maili chache kutoka mjengo wa mwanawe huyo wenye thamani ya pauni Milioni 3.
Wakati nyota huyo wa Manchester City anatanua la gari la kifahari lenye thamani ya pauni 120,000, aina ya Bentley Continental GT, Rose Barwuah anatumia usafiri wa basi maarufu kama Namba 11.
Mara tano kwa wiki, mama huyo anapanda basi hilo kwenda kufanya kazi zake za usafi Cheadle, jirani na Manchester, akiwa analipwa ujira mdogo tu wa pauni kama 6.08 kwa saa.
Nyumbani kwake ni Wythenshawe, eneo ambalo lilitumika kupigia picha za filamu ya Shameless, komedi ya Channel 4.
Mama huyo mwenye umri wa miaka 46 alimtoa kwa wazazi wa wa kufikia Balotelli akiwa ana umri wa miaka miwili, na yeye na mume wake wanaishi kimasikini katika ghorofa la kichovu huko Brescia, Italy.
Krisimasi iliyopita alihamia Manchester ili awe karibu na mwanawe huyo mwenye umri wa miaka 21 sasa.
MWANZO MGUMU: Balotelli alitolewa kwa wazazi wa kufikia akiwa ana umri wa miaka miwili, wakati Rose na mumewe wakiishi kimasikini katika ghorofa la kichovu huko Brescia, Italia
IMETAFSIRIWA KUTOKA; http://www.dailymail.co.uk
0 comments:
Post a Comment