Shiboli |
Na Princess Asia
MSHAMBULIAJI aliyewahi kugombewa na klabu za Simba na Yanga,
kabla ya hajaangukia kwa Wekundu wa Msimbazi, mwaka juzi- Ahmad Ally ‘Shiboli’
ni miongoni mwa wachezaji 11 waliomaliza mikataba yao ya kuichezea timu ya
Coastal Union ya Tanga inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, na sasa wako
huru kujiunga na klabu yoyote.
Kwa mujibu wa Coastal Union, wachezaji wengine ni Ben
Mwalala, Samwel Temu, Francis Busungu, Lawrence Mugia, Daudi Chengula, Godfrey
Mmasa, Mwinyi Abdulrahman, Sabri Ramadhan China, Soud Abdallah na Ramadhan
Wasso.
Uhamisho wa wachezaji kwa msimu huu ulianza Juni 15 mwaka
huu na utamalizika Julai 30 mwaka huu wakati kipindi cha kuanza wachezaji (kwa
wasio wa Ligi Kuu) ni kati ya Juni 15 na 30 mwaka huu.
Kwa klabu za Ligi Kuu kutangaza wachezaji watakaositishiwa mikataba
yao ni kuanzia Juni 15-30 mwaka huu na usajili wa wachezaji unafanyika kuanzia
Juni 15 hadi Agosti 10 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment