Tetesi za Alhamisi magazeti ya Ulaya


LIVERPOOL YAKUBALI HASARA KULIKO GALASA

KLABU ya Liverpool iko tayari kupoteza pauni Milioni 25 kwa mshambuliaji Andy Carroll, kwa mshambuliaji huyo kurejeshwa Newcastle kwa dau la pauni Milioni 10.
KOCHA mpya wa Tottenham, Andre Villas-Boas anamtaka kiungo wa Porto, Joao Moutinho kama mbadala wa Luka Modric. Modric anatarajiwa kuondoka White Hart Lane na Spurs iko tayari kumchukua Moutinho, ambaye aling'ara katika Euro 2012 akiwa na kikosi cha Ureno.
MSHAMBULIAJI wa Porto, Hulk amekanusha kwamba yupo karibu kusaini Chelsea. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye yumo kwenye kikosi cha Olimpiki cha Brazil, anafurahi kubaki Ureno.
Jermain Defoe
Jermain Defoe anaweza kuhamia Reading?
KLABU ya Reading inajiandaa kutoa pauni Milioni 5 kumchukua mshambuliaji wa Tottenham, Jermain Defoe.
KLABU za West Brom na Aston Villa, zote zinamtaka kiungo wa Rennes, Tongo Doumbia.
KLABU ya Brighton imenza maongezi na Arsenal juu ya kumchukua kwa mkopo beki kinda, Ignasi Miquel, lakini wanakabiliwa na upinzani kutoka Barcelona B.
KLABU ya Newcastle imejitosa kwenye mbio za kuwania saini ya winga wa Blackburn, Junior Hoilett - ambaye amemaliza mkataba wake Ewood Park - baada ya pendekezo lake la kwake Borussia Monchengladbach kufeli.
MSHAMBULIAJI wa Tottenham, Rafael van der Vaart anaweza kuondoka kwenda kujiunga na klabu moja Falme za Kiarabu (UAE), baadea ya dili lake la kuhamia Hamburg kushindikana.

CAPELLO KUPEWA URUSI

KOCHA wa zamani wa England, Fabio Capello yupo kwenye nafasi nzuri ya kuchukua nafasi iliyo wazi ya Ukocha wa timu ya taifa ya Urusi, baada ya Harry Redknapp kuamua mwenyewe kujiondoa.
Fabio Capello
Fabio Capello aliacha kazi England Februari
KOCHA wa Wales, Chris Coleman amesema kwamba winga Gareth Bale hayuko fiti kucheza Olimpiki.
KIUNGO mkongwe, David Beckham hatabakia London kwa muda wote wa Michezo ya Olimpiki, baada ya kutemwa kwenye kikosi cha GB. Atarejea Los Angeles kuichezea klabu yake, LA Galaxy.

RODGERS AJITABIRIA UGUMU LIVERPOOL...

KOCHA mpya wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema kwamba anatarajia changamoto kubwa kabla ya kufikia mafanikio katika klabu hiyo ya Anfield.