URA ya Uganda imeichapa Simba SC mabao 2-0, Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam, katika mechi ya Kundi A, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati,
Kombe la Kagame.
URA ilipata mabao yake kupitia Feni Ally dakika ya 11
na ya 90+2.
Katika mchezo huo, Simba ilicheza vizuri, lakini tu
walishindwa kutumia vizuri nafasi walizopata na mabao yote walifungwa wakitoka wao
kushambulia.
Kikwazo kwa Simba leo alikuwa ni beki Derrick Walullya ambaye msimu uliopita alichezea Simba, akatemwa kwa madai kiwango kimeshuka. Aliwatia mfukoni washambuliaji wote wa Simba.
Katika Uwanja wa Chamazi, Azam FC wamelazimishwa sare ya 1-1
na Mafunzo, bao lao lililofungwa na John Bocco ‘Adebayor’dakika ya 26 na Mafunzo walisawazisha kupitia kwa Ally Juma. Katika mchezo
wa kwanza, Chamazi Vita Club imeifunga 7-0 Port ya Djibouti.
0 comments:
Post a Comment