Kiiza akiwa amebebwa na Bahanuzi jana |
Na Prince Akbar
VITA ya kuwania kiatu cha dhahabu cha Klabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati, Kombe la Kagame imezidi kupambana moto, baada ya John Raphael
Bocco ‘Adebayor’ wa Azam FC na Hamisi Kiiza ‘Diego’ wa Yanga kutimiza mabao
matano kila mmoja, hivyo kulingana na Said Bahanuzi ‘Spider Man’ anayeshika
nafasi ya pili, nyuma ya Taddy Etikiama na AS Vita ya DRC, mwenye mabao sita.
Wachezaji wote hao wanne, watakuwa na fursa ya kuongeza
mabao yao Jumamosi, Bocco, Kiiza na Bahanuzi wakicheza fainali kati ya Yanga na
Azam, wakati Taddy akiiongoza AS Vita katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu,
dhidi ya APR ya Rwanda.
John Bocco wa Azam |
Wengine waliomo kwenye kinyang’aniyo hicho ni Suleiman
Ndikumana wa APR mwenye mabao mabao matatu, ambaye pia anaweza kuongeza mabao
yake katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu keso.
Abdallah Juma ‘Dullah Mabao’ wa Simba SC timu yake imetolewa
akiwa ana mabao mawili sawa na Leonel St Preus wa APR, Didier Kavumbagu wa
Atletico, Feni Ali na Robert Ssentongo wa URA.
WANAOONGOZA KWA
MABAO:
Taddy Etikiama AS
Vita 6
Said Bahanuzi Yanga
SC 5
Hamisi Kiiza Yanga
SC 5
John Bocco Azam
FC 5
Suleiman Ndikumana APR 3
Abdallah Juma Simba
SC 2
Leonel St Preus APR 2
Didier Kavumbagu Atletico 2
Feni Ali URA 2
Robert Ssentongo URA 2
0 comments:
Post a Comment