Tetesi za J'nne magazeti ya Ulaya


JUVE YAVAMIA ENGLAND, SASA YAMTAKA LUIS SUAREZ WA LIVERPOOL MBALI NA VAN PERSIE

KLABU ya Juventus inajiandaa kumtwaa mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez katika dili la kutoa fedha na mchezaji.
NAHODHA wa Arsenal, Robin van Persie anajiandaa kufanya mazungumzo na klabu yake, baada ya Washika Bunduki hao, kukataa dau la pauni Milioni 8 kumuuza mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kwa klabu ya Juventus.
KLABU ya Tottenham imetenga dau la pauni Milioni 10 ili kumnasa mshambuliaji mwenye umri wa miaka 22, kutoka klabu ya Chelsea, Daniel Sturridge.
KLABU ya Arsenal imetenga dau la pauni Milioni 12 ili kumtwaa kipa wa kimataifa wa Ufaransa, Hugo Lloris, mwenye umri wa miaka 25, lakini wakati huo huo inakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa klabu za Liverpool na AC Milan.
TAARIFA kutoka Liverpool, zinasema Wekundu hao wa Anfield hawana mpango kabisa na kipa huyo Mfaransa.
Demba Ba
Demba Ba anaweza kugharimu pauni Milioni 7
KLABU ya Liverpool inamtaka mshambuliaji wa Newcastle, Demba Ba, mwenye umri wa miaka 27, ambaye anapatikana kwa dau la pauni Milioni 7, kwa sababu yupo karibu kumaliza mkataba wake.
KLABU ya Chelsea imetenga dau la pauni Milioni 4 kumnasa beki wa kushoto wa Southampton, Luke Shaw. Kinda huyo wa umri wa miaka 16 anainukia vizuri St Mary's na aliichezea mechi yake ya kwanza timu ya wakubwa katika Kombe la  FA dhidi ya Millwall, msimu uliopita.
MCHEZAJI anayewaniwa na klabu za Manchester United na Chelsea, Axel Witsel, mwenye umri wa miaka 23, anaweza kupatakana safari hii, baada ya klabu yake, Benfica kusema itamuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubeligji kwa dau la pauni Milioni 20.
MCHEZAJI Steven Naismith, mwenye umri wa miaka 25, yuko tayari kuzipiga chini West Ham na Blackburn kwa kusaini Everton, akitokea Rangers.

AVB ANATAJWA LEO

KOCHA wa zamani wa Chelsea, Andre Villas-Boas anaweza kutangazwa kuwa kocha mpya wa Tottenham leo.

CASILLAS ALIOMBA DAKIKA ZIPUNGUZWE KUWAHURUMIA ITALIA FAINALI EURO 2012

KIPA wa Hispania, Iker Casillas alimuomba refa amalize mechi ya fainali ya Euro 2012 mapema ili kuwaheshimu wapinzani wao Italia, wasiendelee kupigwa mabao. walikoga 4-0 hadi filimbi ya mwisho na kama dakika zingeongezeka wangetandikwa zaidi.