Tetesi za J'mosi magazeti ya Ulaya
JUVENTUS WAACHANA NA VAN PERSIE
Juventus imezima jaribio lake la kutaka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal, Robin van Persie, ambaye pia anawaniwa na Manchester City na Manchester United.
Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho bado anahaha kuisaidia klabu yake kuiinasa saini ya kiungo mchezeshaji, Luka Modric kutoka Tottenham.
Manchester United inajipanga kufanya jaribio lingine la kumsaini kiungo wa Brazil, Lucas Moura kutoka Sao Paulo.
Arsenal itatakiwa kulipa angalau pauni Milioni 20 kama wanamtaka kiungo Santi Cazorla wa Malaga.
The Gunners, pamoja na hayo, wapo karibu kumnasa kwa mkopo wa muda mrefu kiungo wa Real Madrid, Nuri Sahin.
Liverpool na Arsenal zinakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Lyon katika kuwania saini ya Mamadou Sakho kutoka Paris St Germain.
Kushuka kwa Villarreal kunaweza kuwafanya wampoteze mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Giuseppe Rossi, ambaye kwa sasa anasumbuliwa na maumivu ya goti.
West Ham inataka kuipiga bao Wigan katika kuwania saini ya beki wa Real Mallorca, Ivan Ramis.
Kocha wa Watford, Gianfranco Zola anataka kumsajili mshambuliaji wa QPR, DJ Campbell ili kuisaidia klabu yake kupanda Ligi Kuu.
Kocha wa Blackburn, Steve Kean yuko tayari kumpoteza Junior Hoillett kwa kuwasajili mshambuliaji Simon Cox kutoka West Brom na beki wa Fulham, Aaron Hughes.
WENGER AWAKA KUULIZWA ULIZWA KUHUSU MUSTAKABALI WA VAN PERSIE
Arsene Wenger alipandisha jazba alipoulizwa maswali zaidi kuhusu mustakabali wa mshambuliaji wake na Nahodha wake, Robin van Persie katika klabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment