David Haye akimtupia kitu Chisora katika Uwanja wa Upton Park usiku wa kuamkia leo
AMEKOMA! Kama ingekuwa bongo ndivyo ambavyo Dereck Chisora angeimbiwa
baada ya kutandikwa na bingwa wa zamani wa WBO na WBA uzito wa juu, David Haye,
kwa Knockout (KO) ya raundi ya tano katika pambano la ngumi la uzito wa juu
lililofanyika ujsiku wa kuamkia leo Uwanja wa Upton Park.
Haye alikutana na kibonde haswa ulingoni, kwani alitawala
pambano hilo tangu mwanzo, tena akipigana kwa kujiamini, dhidi ya Chisora ambaye
alipiga ngumi ya kwanza ya kwenye uso wa Haye katika raundi ya tatu.
Chisora ambaye alitamba ataingia katika pambano hilo kama
kichaa na kuahidi kumuangusha Haye raundi ya saba, alijikuta akidondoshwa chini
mara mbili katika raundi ya tano kama gunia la nafaka na pambano likaishia hapo.
Alitandikwa ngumi mbili, ya kulia na ya kushoto upande wa
chini ya shavu la kushoto na kulia, akachanganyikiwa na kuifuata sakafu kwa
mara ya kwanza mapema katika raundi ya tano, ingawa aliinuka baada ya
kuhesabiwa na kuendelea na pambano.
Sekunde chache tu baada ya kurudi mchezoni, Haye alimsogelea
haraka Chisora na kuanza tena kumtandika ngumi mfululizo- alimpiga ngumi tano
mfululizo zilizoingia sawia kwenye taya na usoni, hivyo kumpeleka chini kwa
mara nyingine na huo ndio ukawa mwisho wa pambano.
Ushindi huo unamfanya Haye mwenye urefu wa futi 6 na inchi 3
sasa awe ameshinda mapambano 26 (24 kwa KO) na amepigwa mawili wakati hajatoka
sare, na Chisora amefikisha mapambano manne ya kupigwa, kushinda 15 (9 kwa KO)
na hajatoka sare.
Hilo lilikuwa pambano la kwanza kwa Haye, tangu alitangaza
kustaafu ndondi, baada ya kuchapwa na Vladimir Klitschko Julai 2011 na kupoteza
taji lake la WBA.
Anaenda chini: Chisora akdondoka chini baada ya kuchapwa na from Haye
Amekoma: Chisora anahesabiwa na refa Luis Pabon
Chali: Haye akisogea pembeni baada ya kumbwaga chini Chisora
Machungu ya kipigo: Chisora akilalamika baada ya kupigwa kwa Knockout (KO) na Haye
Mwanzo kabisa: Haye na Chisora wakipewa maelekezo kabla ya pambano.
Nyomi: Umati wa watu ulioshuhudiwa pambano hilo.
SOURCE: http://www.dailymail.co.uk
0 comments:
Post a Comment