Tetesi za Alhamisi magazeti Ulaya
FERGIE ATAMBA; VAN PERSIE ANAKUJA OLD TRAFFORDM, MAN CITY WALIE TU
KOCHA Sir Alex Ferguson amewaambia rafiki zake kwamba Manchester United itazipiku City na Juventus katika mbio za kuwania saini ya Nahodha wa Arsenal, Robin van Persie kwa kukata dau la pauni Milioni 20.
KOCHA Andre Villas-Boas amemuambia Luka Modric, ambaye amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia Real Madrid na Manchester United, hawezi kuondoka Tottenham hadi Spurs ishikishwe pauni Milioni 35.
KLABU ya Chelsea, imefungua tena mazungumzo na Marseille juu ya kumnunua beki wa kulia wa kimataifa wa Hispania, Cesar Azpilicueta, mwenye umri wa miaka 22, ambaye anaweza kuwagharimu pauni Milioni 7.
MSHAMBULIAJI wa klabu ya Borussia Dortmund, Mpoland Robert Lewandowski, mwenye umri wa miaka 23, amefungua milango ya kuhamia Manchester United kwa kusema anataka kucheza Ligi Kuu England.
MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Andy Carroll anataka mustakabali wake utatuliwe hadi wiki ijayo. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England, mwenye umri wa miaka 23, hamekuwa akihusishwa na kuhamia Newcastle, Fulham na Aston Villa.
KLABU za Arsenal na Liverpool zote zinamfuatilia mshambuliaji wa Barcelona, Ibrahim Afellay baada ya Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 26, kuambiwa mustakabali wake uko chini ya kocha mpya , Tito Vilanova.
KLABU ya Fulham imeanza mazungumzo na klabu ya Evian ya Ufaransa, kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Ivory Coast, Yannick Sagbo, mwenye umri wa miaka 24, ambaye anaweza kuwagharimu pauni Milioni 3.5. Kocha Martin Jol pia anawapigia hesabu mchezaji wa Huddersfield, Jordan Rhodes na mkongwe wa Juventus, Vincenzo Laquinta, mwenye umri wa miaka 32.
KLABU ya Fulham inajipanga kumfuata Nigel Reo-Coker, mwenye umri wa miaka 28, ambaye kwa sasa ni mchezaji huru, baada ya kuondoka Bolton kufuatia kushuka daraja.
KLABU ya Arsenal imeambiwa iongeze dau lake kwa ajli ya kumnunua Mfaransa, M'Baye Niang, mwenye umri wa miaka 17, baada ya ofa yao ya awali kupigwa chini na Caen.
KLABU ya Newcastle iko nyuma ya Inter Milan na Napoli katika mbio za kuwania saini ya beki wa kimataifa wa Ufaransa, anayechezea klabu ya Lyon, Aly Cissokho, mwenye umri wa miaka 24.
KLABU ya Leeds inajiandaa kumsajili mshambuliaji Luke Varney, mwenye umri wa miaka 29, kutoka Portsmouth, lakini watatakiwa kuilipa Derby pauni 300,000 .
WENGER SASA AKUBALI KUJADILI NA
THEO WALCOTT MKATABA MPYA
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger sasa yuko tayari kufungua mazungumzo ya kujadili mkataba mpya na winga wa England, Theo Walcott, ambaye mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu ujao.
KOCHA Gary Neville amesema kocha wa kikosi cha Olimpiki cha Uingereza, Team GB, Stuart Pearce alikuwa sahihi kumtema rafiki yake, David Beckham kwenye kikosi cha michuano hiyo.
KLABU ya Blackburn imemchukua kwa ajili ya kumfanyia majaribio mshambuliaji wa kimataifa wa Mali, Garra Dembele mwenye umri wa miaka 26 ambaye kwa sasa anachezea Freiburg.
BEKI wa zamani wa Chelsea, Alex anaamini Andre Villas-Boas alistahili kupewa muda zaidi Stamford Bridge - licha ya kufukuzwa kwa Mreno huyo.
0 comments:
Post a Comment