Tetesi za J'tano magaazeti ya Ulaya
SPURS WANASA KIPA LA UFARANSA
KLABU ya Tottenham ipo karibu kumsajili kipa wa kimataifa wa Ufaransa, Hugo Lloris kutoka klabu ya Lyon - lakini watatakiwa kukuza dau lao kutoka pauni Milioni 3 hadi Milioni 15.
KLABU ya West Ham inatumai kiungo Kevin Nolan - rafiki wa karibu wa Andy Carroll anaweza kuondokaLiverpool kwenda Upton Park kwa mkopo.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa England, Andy Carroll atapingana na uamuzi wa kumtoa kwa mkopo msimu ujao na kuamua kubaki Anfield kupambana kugombea namba katika kikosi cha Brendan Rodgers.
KIPA wa QPR, Paddy Kenny atahusishwa na Neil Warnock kwa mara ya tatu baada ya kukubali ofa ya pauni 400,000 kuhamia Leeds.
KLABU ya Hamburg inamfukuzia Rafael van der Vaart, mwenye umri wa miaka 29, na kocha mpya wa Tottenham Andre Villas-Boas yupo tayari kumuuza mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi.
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Wigan, Hugo Rodallega, mwenye umri wa miaka 26, yupo karibu kusaini Fulham licha ya kwamba anatakiwa pia na Everton.
KLABU ya AC Milan imefufua nia yake ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester City, Carlos Tevez.
MCHEAZAJI anayetakiwa na klabu ya Newcastle, Vurnon Anita ameambiwa anaweza kuondoka Ajax safari hii- ikiwa The Magpies watawalipa mabingwa hao wa Uholanzi pauni Milioni 8.
NYOTA wawili wa klabu ya Wolves, Steven Fletcher na Matt Jarvis wanaweza kuihama klabu hiyo iliyoshuka daraja.
WINGA wa klabu ya Sunderland, Ahmed Elmohamady anawaniwa na klabu ya Hull City.
DI MATTEO ATOA BEKI LA MAANA
KOCHA wa Chelsea, Roberto Di Matteo yuko tayari kumruhusu beki kinda wa 'bei chafu' , Nathaniel Chalobah, mwenye umri wa miaka 17, kwenda kwa mkopo katika klabu za Ligi Daraja la Kwanza, baada ya kufanya vema akiichezea timu ya vijana ya taifa ya England katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya kwa vijana chini ya umri wa miaka 19.
KOCHA wa zamani wa Tottenham, Harry Redknapp hana mpango na nafasi iliyo wazi ya kocha wa timu ya taifa ya Urusi, licha ya kuingia kwenye orodha ya watu 13 wa mwisho wanaofikiriwa kwa kibarua hicho.
FAMILIA ya Glazer kwa mara nyingine imejikuta mtatani ikishutumiwa na wachambuzi wa soka England, kwa ubahili wa kutoa fedha za kusajili Manchester United, baada ya hasara waliyoipata msimu wa 2011-12.
0 comments:
Post a Comment