Na Prince Akbar
TIMU ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Coastal Union ya
Tanga, leo imefanikiwa kuingia fainali ya michuano ya Rollingston, baada ya kuwafunga
mabingwa watetezi, Ruvu Shooting mabao 2-1 nchini Burundi.
Mabao yote ya Coastal yalitiwa kimiani na Mohamed Miraj,
wakati bao la Ruvu waliotwaa ubingwa wa michuano hiyo mwaka jana mjini Arusha,
lilitiwa kimiani na Said Hussein.
Kwa matokeo hayo, Coastal itamenyana na Ecofoot ya Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ambayo katika Nusu Fainali nyingine leo,
waliitoa Mjini Magharibi ya Zanzibar kwa mabao 2-1 pia.
Mabao ya Ecofoot
yalitiwa kimiani na Sais Kabamba na Shukuru Hamisi, wakati bao la kufutia machozi
la Mjini Magharibi lilitiwa kimiani na Omar Tamim. Sasa, Mjini Magharibi itamenyana
na Ruvu katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu na Coastal itamenyana na Ecofoot
katika mechi ya kusaka bingwa mpya wa michuano hiyo keshokutwa.
0 comments:
Post a Comment