Chuji |
Na Prince Akbar
ATHUMANI Iddi ‘Chuji’, kiungo wa Yanga amesema kwamba
mashabiki wasikatishwe tamaa na matokeo ya timu hiyo katika mchezo wa kwanza wa
Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame ambao timu hiyo
ilifungwa 2-0 na Atletico ya Burundi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam juzi.
Chuji ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba mchezo uliwakataa
siku hiyo na hilo huwa linatokea kwenye soka, lakini anaamini timu yao ni bora
na itabeba Kombe mwisho wa mashindano.
“Mpira ulikataa tu, inatokea hiyo. Kila tunachokifaya
kinatakaa, hadi tukawa tunashangaa, lakini nasaema mashabiki wasikate tamaa, sisi
timu yetu nzuri na ina mafundi wengi na tunajiamini kabisa, hili Kombe
tunabeba,”alisema Chuji.
Yanga itamenyana na Waw Salaam ya Sudan Kusini kesho, mechi
itakayotanguliwa na mchezo kati ya Atletico na APR ya Rwanda, iliyowafunga
Wasudan 7-0 katika mchezo wa kwanza.
0 comments:
Post a Comment