Tetesi za Alhamisi magazeti Ulaya


CAVANI ATUA CHELSEA NA MKEWE


WAKALA wa mshambuliaji wa Napoli, Edinson Cavani amesema mshambuliaji huyo wa Uruguay, mwenye umri wa miaka 25, atakuwa wazi kuhamia Chelsea baada ya mkewe kumfuata England kuungana naye kwenye MIchezo ya Olimpiki.
Edinson Cavani
Edinson Cavani amefunga mabao 59 katika mechi 86 Napoli
KOCHA Alan Pardew amesistiza Newcastle itamchukua Andy Carroll ikiwa tu Liverpool itakubali kupata hasara na hawawezi kutoa pauni Milioni 20 wanazotaka wao.
RAIS wa Sao Paulo amesema kwamba mpango wa Manchester United kumsajili kinda wao mwenye umri wa miaka 19, winga Lucas Moura unaweza kufufuka.
Everton na West Ham imepewa matumaini ya kufufuka kwa mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Inter Milan, Luc Castaignos,  mwenye umri wa miaka 19, baada ya klabu ya FC Twente ya Uholanzi, kusema hawajakamilisha usajili wa mchezaji huyo.
KIUNGO Frank Lampard, mwenye umri wa miaka 34, amesema yuko tayari kuanza majadiliano ya kusaini mkataba mpya Chelsea kwa kipindi chote kilichobakia cha maisha yake ya soka.
KLABU ya West Ham inataka kumsajili tena beki wa zamani, James Collins, mwenye umri wa miaka 28, kutoka Aston Villa kwa dau la pauni Milioni 2.
KLABU ya Juventus inamfukuzia mshambuliaji wa Manchester City, Edin Dzeko, ambaye bado hana uhakika sana wa namba kwenye 11 wa kwanza Etihad.
KLABU ya Chelsea imeibua mpango mpya wa pauni Milioni 9 kumsajili mshambuliaji wa Wigan, Victor Moses, mwenye umri wa miaka 21, ambaye yupo katika mwaka wa mwisho kwenye mkataba wake DW Stadium.
KOCHAZ mpya wa Swansea, Michael Laudrup anataka kumsajili nyota wa kimataifa wa Venezuela, Miku,   mwenye umri wa miaka 26, kutoka Getafe.

SWANSEA SASA BIFU NA LIVERPOOL


KLABU ya Swansea imeiwakia Liverpool kwa kukiuka  makubaliano yaliyofikiwa kwa maandishi kutojaribu kutaja kusajili wachezaji wao kwa miezi 12 baada ya Brendan Rodgers kujikunga nao, kwa kuomba kumsajili kiungo Joe Allen.