Tetesi za J'mosi magazeti ya Ulaya
MAN CITY WAWEKA KIASI CHA MBOGA KUMNASA VAN PERSIE
KLABU ya Manchester City itaweka dau la pauni Milioni 15 kwa ajili ya mshambuliaji wa Arsenal, Robin Van Persie, mwenye umri wa miaka 28, lakini Barcelona na Paris Saint-Germain pia zinamtaka mchezaji huyo, ambaye amekataa kusaini mkataba mpya katika klabu yake.
VITA ya kuwania saini ya Nahodha wa Arsenal, Robin van Persie zimeshika kasi, baada ya AC Milan nayo kujitosa rasmi kuwania saini ya mfungaji huyo bora wa Ligi Kuu England, mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi.
KOCHA Brendan Rodgers yupo karibu kumnasa mshambuliaji wa Roma, Fabio Borini, mwenye umri wa miaka 21, ambaye atakuwa mchezaji wa kwanza kumsaini tangu aanze kazi Liverpool, baada ya mazungumzo na klabu hiyo Iya talia kuhusu mpachika mabao huyo.
MSHAMBULIAJI wa England, Jermain Defoe, mwenye umri wa miaka 29, ameambiwa hawezi kuondoka Tottenham na kocha mpya wa klabu hiyo, Andre Villas-Boas.
KIUNGO Luka Modric, mwenye umri wa miaka 26, yupo karibu kukubali dau la pauni Milioni 28 kuondoka White Hart Lane kuhamia Real Madrid.
KLABU za Aston Villa na Sunderland zinamtaka mchezaji mwenye thamani ya pauni Milioni 9, beki wa Real Mallorca, Ivan Ramis, mwenye umri wa miaka 27, ambaye alikataa kujiunga na Everton miaka miwili iliyopita. FHabari kamili: the Sun
KLABU ya Newcastle imepiga chini mpango wa kumsaini winga wa Blackburn, Junior Hoilett, mwenye umri wa miaka 22, lakini ipo karibu kumsajili kinda wa timu ya taifa ya vijana ya Australia chini ya miaka 20, Curtis Good, mwenye umri wa miaka 19, kutoka Melbourne Heat.
KLABU ya Tottenham inajipanga kuwapiku wapinzani wao, Arsenal katika kuwania saini ya kipa wa Italia, Emiliano Viviano, mwenye umri wa miaka 26, ambaye anamilikiwa kwa pamoja na klabu za Serie A, Inter Milan na Palermo.
MWANASOKA wa kimataifa wa Ubelgiji, Jan Vertonghen, mwenye umri wa miaka 25, atakuwa na mazungumzo na Ajax kuzungumzia suala lake la kuhamia Tottenham kwa dau la pauni Milioni 9, ambalo kwa sasa linaonekana kupepesuka.
TOTTENHAM Hotspur inataka kujaribu kwa mara ya tatu kumsajili mshambuliaji wa Internacional, Leandro Damiao, mwenye umri wa miaka 22, baada ya kuona klabu yake ya Brazil, imesajili mshambuliaji mbadala wake, Diego Forlan wa Uruguay.
MCHEZAJI wa Internacional, Oscar , mwenye umri wa miaka 20, amesema hana mpango wa kuihama klabu yake hiyo ya Brazil, licha ya Tottenham kumtengea dau la pauni Milioni 10 kiungo huyo.
KOCHA AFUKUZA WANANE
KOCHA wa Preston, Graham Westley, mwenye umri wa miaka 44, anashutumiwa kuwatumia meseji wachezaji wake wanane, akiwaambia wakae mbali kabisa na mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya.
KLABU ya Manchester City itatwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, kama Robin van Persie atahamia Etihad Stadium, kwa mujibu wa beki wa Blues, Kolo Toure.
BEKI wa zamani wa Arsenal, Sol Campbell, mwenye umri wa miaka 37, ameiambia klabu yake hiyo ya zamani njia pekee ya kumbakisha Van Persie ni kufanya usajili wa wachezaji wapya wa pauni Milioni 100.
MCHEZAJI wa zamani wa Arsenal, And Nigel Winterburn, amekuiwa nyota mwingine wa zamani wa klabu hiyo, kuionya klabu yake kwamba itakuwa kibonde katika Ligi Kuu England, iwapo itaendelea na ubahili wake wa kununua wachezaji.
MWENYEKITI wa Arsenal, Peter Hill-Wood amesema kushambulia sera za klabu hiyo ni upumbavu.
MMILIKI wa QPR na Mwenyekiti, Tony Fernandes amemuonya Joey Barton, mwenye umri wa miaka 29, asirudie kosa alilolifanya hadi akapewa kadi nyekundu Manchester City katika mechi ya mwisho ya msimu uliopita wa Ligi Kuu England.
NAHODHA wa Manchester United, Nemanja Vidic, mwenye umri wa miaka 30, anatumai kuwa fiti kuelekea mwanzoni mwa msimu mpya, baada ya kurejea kwenye mazoezi ya kikosi cha kwanza.
ANELKA KUREJEA ENGLAND
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Anelka, mwenye umri wa miaka 33, anataka kurejea Ligi Kuu England baada ya kuhitilafiana na klabu ya Shanghai Shenhua.
0 comments:
Post a Comment