Wachezaji wa Azam |
Na Prince Akbar
MICHUANO ya Kombe la Urafiki, inayoandaliwa na Chama cha
Soka Zanzibar (ZFA), inatarajiwa kuendelea leo kwa mchezo kati ya Super Falcon na
Jamhuri ya Pemba kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mechi nyingine ya kundi hilo, B ingekuwa kati ya Yanga na
Zanzibar All Stars, lakini ZFA imeiengua Yanga kwenye michuano hiyo kwa
kupeleka timu B, badala ya timu A.
Mechi za Kundi A zitaendelea kesho, kwa Azam kujaribu kusaka
ushindi wa kwanza kwenye michuano hiyo mbele ya Mafunzo, baada ya kucheza mechi
mbili za awali bila kushinda.
Mabingwa wa Tanzania Bara, Simba SC wao watakuwa mikononi
mwa timu ambayo ni tishio kwenye michuano hiyo, Karume Boys. Mechi hizo za
kesho ndizo zitaamua timu za kuingia Nusu Fainali kwenye Kundi hilo.
Karume ina pointi sawa na Simba SC, nne kila moja lakini
inazidiwa bao moja la kufunga na Wekundu hao wa Msimbazi.
Katika mechi za Kundi A jana, Simba SC walishindwa kuwafunga
Azam FC licha ya kucheza pungufu, baada ya kutoka sare ya 1-1.
Simba ilitangulia kupata bao dakika ya 35 kupitia kwa
mshambuliaji wake iliyemsajili kutoka Dong Tam Long An ya Vietnam, Danny
Mrwanda, lakini Azam ilisawazisha kupitia kwa George Odhiambo ‘Blackberry’
dakika ya 45.
Katika mechi hiyo, iliyokuwa kali nay a kusisimua, Abdulhalim
Humud alipewa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu dakika ya 52 na kutolewa
nje, hivyo Azam kubaki pungufu ya mchezaji mmoja uwanjani.
Katika mechi yake ya kwanza, Simba SC ilianza vyema baada ya
kuifunga Mafunzo mabao 2-1, wakati Azam ililazimishwa sare ya 1-1 na U23,
Karume Boys.
Simba sasa inaongoza kundi hilo kwa pointi zake nne, mabao
matatu ya kufunga na mawili ya kufungwa, wakati Mafunzo ni ya pili kwa pointi
zake nne, mabao mawili ya kufunga na moja la kufungwa na Azam FC ni ya tatu kwa
pointi zake mbili, wakati Mafunzo inashika mkia baada ya kufungwa mechi zote mbili.
0 comments:
Post a Comment