Kikosi cha Azam leo |
Kikosi cha Tusker leo |
Na Prince Akbar
AZAM na Mafunzo ya Zanzibar zimefuzu kuingia Robo Fainali ya
Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, kufuatia Wana Chamazi kutoka sare ya
bila kufungana na Tusker ya Kenya mchana wa leo, Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Timu zote za Kundi B zimemaliza zikiwa na pointi mbili kila
moja, lakini Tusker haina bao baada ya kutoa sare ya bila kufungana mechi zote
na Mafunzo na Azam wanabebwa na sare ya kufungana bao 1-1 katika mechi ya
kwanza kabisa ya kundi hilo, Uwanja wa Chamazi.
Tusker walilazimika kucheza pungufu tangu dakika ya 51,
baada ya kipa wao Boniphace Olouch kutolewa nje kwa kadi nyekundu na refa Issa
Kagabo wa Rwanda kwa kumchezea rafu John Bocco wakati anakwenda kufunga.
Andrew Mutunga alitoka na akaingia kipa wa akiba Samuel Odhiambo
na katika kuogeza kasi ya mashambulizi, Azam walimpumzisha Kipre Tchecthe
akaingia Mrisho Ngassa.
Katika mchezo huo, kikosi cha Azam kilikuwa;
Deo Munishi ‘Dida’, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Ibrahim Shikanda, Jospeh
Owino, Kipre Ballou, Kipre Tchetche, Ibrahim Mwaipopo, John Bocco, Ramadhan
Chombo na Hamisi Mcha ‘Vialli’.
Benchi; Mwadini Ally, Samir Hajji Nuhu, Said Mourad, George
Odhiambo ‘Blackberry’, Mrisho Ngassa, Jabir Azizi na Gaudence Mwaikimba.
Kocha; Stewart Hall (Uingereza)
Tusker; Boniface Oluouch, Joseph Shikokoti, Jockins Atudo,
Humphrey Okoti, David Ochieng, Joseph Mbugi, David Nyanzi Makumbi, Jerry Santo,
Andrew Murunga, Peter Opiyo na Joshua Oyoo.
Benchi; Samuel Odhiambo, Luke Ochieng, Maurice Odipo, Dennis
Mukaisi, Fredrcik Onyango, Patrick Kagogo, Obadia Ndege, Joseph Mbugi na Allan
Kateregga.
Kocha; Samuel Omollo
0 comments:
Post a Comment