Azam Academy mazoeini Chamazi |
Na Prince Akbar
AZAM Academy leo imetolewa katika michuano ya vijana chini
ya umri wa 17, Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Rollingston inayoendelea
nchini Burundi, baada ya kufungwa na Mjini Magharibi ya Zanzibar 1-0.
Bao hilo pekee la Mjini Magharibi, lilipatikana kwa penalti dakika
ya 89. Katika hatua hiyo, Tanzania imeonyesha kuwa na msingi mzuri wa soka ya
vijana kutokana na kufanikiwa kuingiza timu sita katika hatua ya Robo Fainali
ya michuano hiyo, ambayo awali ilikuwa ikifanyika mjini Arusha.
Timu nyingine zilizoingia hatua hiyo ni JKT Ruvu ya Pwani,
Mjini Magharibi ya Zanzibar, Coastal Union ya Tanga na Bishop Dunhill na
Rollingston za Arusha.
Robo Fainali zote zimechezwa leo katika viwanja viwili
tofauti, Aigle Noir ya Burundi imemenyana na JKT Ruvu, Ecofoot ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ikimenyana na Bishop Dunhill Uwanja wa Gisenyi,
wakati Rollingston imecheza na Coastal Union Uwanja wa Nyanza. Ruvu shooting, Coastal Union nazo zimeingia Nusu Fainali pamoja na Ecofoot. Nusu Fainali zitachezwa kesho.
0 comments:
Post a Comment