Humud alipewa kadi nyekundu mapemaa, lakini Simba hawakutumia nafasi |
Na Prince Akbar
MABINGWA wa Tanzania Bara, Simba SC usiku huu wameshindwa
kuwafunga washindi wa pili wa ligi hiyo, Azam FC licha ya kucheza pungufu
katika mchezo wa Kundi A wa Kombe la Urafiki, kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar,
baada ya kutoka sare ya 1-1.
Simba ilitangulia kupata bao dakika ya 35 kupitia kwa
mshambuliaji wake iliyemsajili kutoka Dong Tam Long An ya Vietnam, Danny Mrwanda,
lakini Azam ilisawazisha kupitia kwa George Odhiambo ‘Blackberry’ dakika ya 45.
Abdulhalim Humud alipewa kadi ya pili ya njano na kuwa
nyekundu dakika ya 52 na kutolewa nje, hivyo Azam kubaki pungufu ya mchezaji
mmoja uwanjani.
Katika mechi yake ya kwanza juzi, Simba SC ilianza vyema
baada ya kuifunga Mafunzo mabao 2-1, wakati Azam ililazimishwa sare ya 1-1 na
U23, Karume Boys.
Simba sasa inaongoza kundi hilo kwa pointi zake nne, mabao
matatu ya kufunga na mawili ya kufungwa, wakati Azam FC ni ya pili kwa pointi
zake mbili
Simba; Juma Kaseja, Haruna Shamte, Paul Ngalema, Lino
Masombo, Shomary Kapombe, Amri Kiemba/Edward Chirtopher, Mwinyi Kazimoto/Salim
Kinje, Mussa Mudde/Jonas Mkude, Abdallah Juma, Kanu Mbivayanga/ Uhuru Suleiman
na Danny Mrwanda/Abdallah Seseme.
Azam: Deo Munishi ‘Dida’, Samir Hajji Nuhu, Ibrahim Shikanda,
Said Mourad, Joseph Owino, Abdulhalim Humud, Kipre Herman Tcheche, Kipre Michael
Balou, Ramadhan Chombo ‘Redondo’, Gaudence Mwaikimba na George Odhiambo ‘Blackberry’/Hamisi
Mcha.
Katika mchezo wa awali wa kundi hilo jioni ya leo, Karume Boys
ilishinda 1-0 dhidi ya Mafunzo, bao pekee la Nassor matter dakika ya 45.
Aidha, mapema jioni ya leo, Yanga ilirudishwa nyumbani Dar
es Salaam, kwa kitendo cha kupeleka timu B badala ya timu A.
Yanga ilikuwa Kundi B pamoja na Jamhuri, Falcon na All
Stars. Jana ilifungwa 3-2 na Jamhuri katika mchezo wao wa kwanza.
0 comments:
Post a Comment