MASHINE; Sunzu, ataibeba simba na leo? |
Na Prince Akbar,
MICHUANO ya Kombe la Urafiki visiwani Zanzibar, leo inafikia
hatua ya Nusu Fainali kwa mechi mbili kupigwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC watacheza na Zanzibar All
Stars kuanzia saa 2:00 usiku, wakati Azam FC watamenyana na Super Falcon
kuanzia saa 10:30 jioni.
Azam na Simba, zote zimefuzu kutoka Kundi A wakati All Stars
na Falcon zimetokea Kundi B, lililokuwa na Yanga pia, ambayo iliondolewa kwa
kupeleka watoto.
Simba SC ni mabingwa wa Bara, Falcon ni mabingwa wa Zanzibar,
Azam FC ni mabingwa wa Kombe la Mapinduzi na washindi wa pili wa Ligi Kuu ya
Bara wakati Falcon inaundwa na mseto wa wachezaji nyota wa Zanzibar.
Katika mechi yake ya mwisho ya Kundi A, Simba iliifunga kwa
taabu Karume Boys 1-0, bao pekee la mshambuliaji wake Mzambia, Felix Mumba Sunzu
Jr, wakati Azam iliifunga Mafunzo 3-2.
ADEBAYOR WA CHAMAZI; Ataibeba Azam leo? |
Kuna uwezekano mkubwa Simba na Azam zikakutana katika
Fainali Jumatano, kwani zinapewa nafasi kubwa ya kushinda mechi zao leo, ingawa
pia haitarajiwi kuwa kazi nyepesi kwani timu za Zanzibar nazo zimeimarika siku
za karibuni.
Katika mchezo wa leo, huanda kocha wa Simba Profesa Milovan
Cirkovick akapanga kikosi hiki; Juma Kaseja, Haruna Shamte, Paul Ngalema, Lino
Masombo, Shomary Kapombe, Amri Kiemba/Edward Chirtopher, Mwinyi Kazimoto/Salim
Kinje, Mussa Mudde/Jonas Mkude, Felix Sunzu/Abdallah Juma, Kanu Mbivayanga/
Uhuru Suleiman na Danny Mrwanda/Abdallah Seseme.
Kwa upande wa Azam, inawezekana Stewart Hall, akawapanga:
Deo Munishi ‘Dida’, Samir Hajji Nuhu, Ibrahim Shikanda, Said Mourad, Joseph
Owino, Abdulhalim Humud, Kipre Herman Tcheche, Kipre Michael Balou, Ramadhan
Chombo ‘Redondo’, Gaudence Mwaikimba na George Odhiambo ‘Blackberry’/Hamisi
Mcha.
0 comments:
Post a Comment