Kocha wa Azam, Muingereza Stewart Hall, ataendelea kuwa simu ya vigogo wa soka Tanzania? |
Na Prince Akbar
MICHUANO ya Kombe la Urafiki, inayondaliwa na Chama cha Soka
Zanzibar, inatarajiwa kuendelea leo kwa mchezo mkali na wa kusisimua kati ya
mabingwa wa Tanzania Bara, Simba SC na Azam FC kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mchezo huo wa Kundi A unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua
kutokana na ukweli kwamba Azam ndio washindi wa pili wa Ligi Kuu.
Aidha, mechi baina ya timu hizo siku za karibuni zimekuwa zenye
upinzani mkali na ikizingatiwa timu zote zitashiriki Klabu Bingwa Afrika Mashariki
na Kati, Kombe la Kagame- basi kila upande utataka kuwatia moyo mashabiki wake.
Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga ‘Mr. Liverpool’ alisema
jana kwamba wana matumaini ya kuifunga Azam FC leo, ili wawadhihirishie wao ndio
‘Baba ya soka Tanzania’.
Kwa upande wake, Katibu wa Azam FC, Nassor Idrisa alisema
nao wako vizuri na wamejipanga vema kuifunga Simba SC.
Katika mechi yake ya kwanza juzi, Simba SC ilianza vyema
baada ya kuifunga Mafunzo mabao 2-1, wakati Azam ililazimishwa sare ya 1-1 na
U23, Karume Boys.
Mabao yote ya Wekundu wa Msimbazi yalitupiwa nyavuni na
mshambuliaji mpya, aliyesajiliwa kutoka Ruvu Shooting ya Pwani, Abdallah Juma,
ambaye amepokewa Simba kama Emmanuel Gabriel mpya. Dullah alifunga mabao hayo
dakika ya 27 na 44, yote akiunganisha pasi za kuingo kutoka Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Patrick Kanu Mbivayanga, wakati Mafunzo walipata
bao lao kufutia machozi dakika ya 80, mfungaji Jaku Joma.
Azam wao juzi walilazimika kusubiri hadi dakika ya 79 kupata
sare ya 1-1 kwa bao la mshambuliaji wake kutoka Ivory Coast, Kipre Tcheche,
baada ya Karume Boys kupata bao la kuongoza dakika ya 45 kwa njia ya penalti,
mfungaji Ibrahim Hamisi.
Katika mechi za kwanza za Kundi A jana, Yanga ya Dar es
Salaam pia, ilifungwa kwa taabu mabao 3-2 na Jamhuri ya Pemba kwenye Uwanja wa
Amaan, Zanzibar.
Yanga ambayo imepeleka wachezaji wake wa kikosi cha vijana
visiwani humo, hadi mapumziko, ilikuwa tayari nyuma kwa mabao 2-1.
Lakini kipindi cha pili, Yanga B walikuja juu na kucheza
soka ya kuvutia, ingawa waliishia kukosa mabao ya wazi kabla ya kupata moja na
wapinzani wao wakipata moja zaidi pia .
Kocha wa Simba, Mserbia Milovan Cirkock, ataendelea kucheka leo> |
Mabao ya Jamhuri yalitiwa kimiani na Ally Salum dakika ya
34, Abdallah Othman dakika ya 45 na Mohamed Omar dakika ya 69, wakati mabao ya
Yanga yalifungwa na Hamisi Shaaban dakika ya 17 na Nofteli Mwansasu dakika ya
77.
Katika mchezo wa Kundi hilo uliotangulia hiyo jana, Super
Falcon ilitoka sare ya kufungana mabao 2-2 na Zanzibar All Stars. Mabao ya Falcon
yalifungwa na Deo Cassian dakika ya 12 na 25, wakati ya All Stars yalitupiwa
nyavuni na Ahmad Malik dakika ya 46 na Twaha Mohamed dakika ya 81.
0 comments:
Post a Comment