Azam FC |
Na Prince Akbar
SIMBA inacheza mechi ya mwisho ya Kundi A, Klabu Bingwa
Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mchezo ambao unatarajiwa kuwa mkali na wa
kusisimua na wakati huo huo Azam watacheza na Tusker ya Kenya katika Kundi B.
Timu zote, Vita inayofundishwa na kocha wa zamani wa Yanga,
Raoul Jean Pierre Shungu na Simba inayofundishwa na Mserbia Milovan Cirkovick, zimekwishafuzu
Robo Fainali, lakini mchezo wa leo unaweza tu kurekebisha tu msimamo wa kundi
hilo, timu ipi iwe ya pili na ipi iwe ya tatu,
Simba SC |
Simba SC walijihakikishia kufuzu Robo Fainali jana baada ya
vinara wa kundi hilo, URA kuichapa Ports ya Djibouti mabao 3-1. Ports iliyoanza
kwa kufungwa 7-0 na AS Vita, juzi pia ilifungwa na Simba mabao 3-0 hivyo kuaga
mashindano kwa kupoteza mechi zote .
Shujaa wa Simba katika mchezo huo, alikuwa mshambuliaji mpya
kutoka Ruvu Shooting ya Pwani, Abdallah Juma aliyeingia kuchukua nafasi ya Amri
Kiemba mwanzoni mwa kipindi cha pili aliyefunga mabao mawili dakika za 60 na 73
na Felix Mumba Sunzu Jr. aliyefunga moja kwa penalti dakika ya 64
Kinara wa mabao Simba SC; Abdallah Juma 'Dullah Mabao' |
Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika bila nyavu za
Ports kutikisika, na katika kipindi hicho Sunzu, mshambuliaji wa kimataifa wa
Zambia, alipoteza nafasi tatu za wazi mno, za kufunga mabao akiwa amebaki yeye
na kipa, Kalid Ali Moursal.
Mabadiliko yaliyofanywa na kocha Mserbia, Milovan Cirkovick
kipindi cha pili kuwaingiza Juma Nyosso kuchukua nafasi ya Haruna Shamte,
Abdallah Juma aliyechukua nafasi ya Kiemba na baadaye Uhuru Suleiman kuchukua
nafasi ya Haruna Moshi ‘Boban’ yaliisaidia Simba.
Kiungo wa Azam Gerorge Odhiambo 'Blackberry' |
Matokeo hayo, yanaifanya Simba iwe na pointi tatu baada ya
kucheza mechi mbili na sasa inashika nafasi ya tatu kwenye Kundi A, nyuma ya
URA yenye pointi tisa na AS Vita yenye pointi tatu na wastani mzuri wa mabao.
Simba inamaliza na AS Vita ya DRC, mechi ambayo itakuwa kali kwa sababu timu
zote zina pointi sawa.
Mechi za Kundi C zilimalizika jana na Atletico wameongoza
kundi, Yanga wa pili na APR wa tatu, timu zote zikifuzu Robo Fainali.
Mechi za Kundi B zinahitimishwa pia leo kwa mchezo
utakaotangulia saa 8:00 mchana kati ya Tusker ya Kenya na Azam FC ya Dar es
Salaam.
Tusker iliyotoka sare ya bila kufungana na Mafunzo ya
Zanzibar juzi, imelifanya kundi hilo lizidi kuwa gumu na katika mchezo wa leo, timu
itakayoshinda moja kwa moja itaungana na Mafunzo kutinga Robo Fainali.
Hatima ya Mafunzo kucheza au kutocheza Robo Fainali
inashikiliwa na mechi hiyo, kwani iwapo timu hizo zitatoka sare ya kuanzia
mabao 2-2 zitakwenda zote Nane Bora na wawakilishi wa Zanzibar watarejea
nyumbani.
MISIMAMO YA MAKUNDI KOMBE LA KAGAME:
KUNDI A:
P W D L GF GA GD Pts
URA 3 3 - - 8 2 6 9
AS Vita 2 1 - 1 8 3 5 3
Simba 2 1 - 1 3 2 1 3
Ports 3 - - 3 1 10 -9 -
KUNDI B:
P W D L GF GA GD Pts
Mafunzi 2 - 2 - 1 1 - 2
Azam FC 1 - 1 - 1 1 - 1
Tusker FC 1 - 1 - - - - 1
KUNDI C
P W D L GF GA GD Pts
Atletico 3 2 1 - 7 - 7 7
Yanga 3 2 - 1 9 3 6 6
APR 3 1 1 1 7 2 5 4
Waw 3 - - 3 - 19 -19 0
0 comments:
Post a Comment