Na Prince Akbar
AZAM FC imenusurika kulala mbele ya timu ya taifa ya vijana
chini ya umri wa miaka 23 (U23) ya Zanzibar, Karume Boys baada ya kulazimisha
sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Urafiki jioni
hii Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Karume Boys walipata bao la kuongoza dakika ya 45 kwa njia penalti,
mfungaji Ibrahim Hamisi.
Kipindi cha pili Azam walikuja juu na dakika ya 79
wakafanikiwa kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wa Ivory Coast, Kipre
Tcheche (pichani kulia).
Mechi nyingine ya Kundi A kati ya mabingwa wa Tanzania Bara,
Simba SC na mabingwa wa Zanzibar, Mafunzo inaanza muda huu kwenye Uwanja huo
huo wa Amaan, Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment