Kikosi cha Yanga leo |
Kikosi cha Azam leo |
Na Prince Akbar
FAINALI ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati,
Kombe la Kagame, kati ya Yanga SC na Azam FC inaendelea hivi sasa Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa mechi ya kusaka mshindi wa tatu,
AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ikiifunga 2-1 APR ya Rwanda.
Mechi kati ya Yanga na Azam inachezeshwa na refa Thierry
Nkurunzinza kutoka Burundi, akisaidiwa na Simba Honore wa Rwanda na Peter
Sabatia wa Kenya, wakati mezani atakaa Issa Kagabo wa Rwanda, Kamisaa Hassan
Amir wa Somalia na Mtathmini wa marefa ni Anangwe Robert wa Kenya.
Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Stefano Mwasyika, Oscar
Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Rashid
Gumbo, Haruna Niyonzoma, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na David Luhende. Benchi;
Shamte Ally, Juma Seif, Ladislaus Mbogo, Idrisa Assenga na Jerry Tegete.
Azam FC; Deo Munishi ‘Dida’, Ibrahim Shikanda, Erasto Nyoni,
Said Mourad, Aggrey Morris, Jabir Aziz, Kipre Tcheche, Salum Abubakar, John
Bocco ‘Adebayor’, Ibrahim Mwaipopo na Ramadhan Chombo ‘Redondo’. Benchi;
Mwadini Ally, Samir Haji Nuhu, Joseph Owino, George Odhiambo, Mrisho Ngassa,
Khamis Mcha ‘Vialli’ na Gaudence Mwaikimba.
Katika mchezo uliotangulia wa kusaka mshindi wa tatu, AS ya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) iliifunga APR ya Rwanda mabao 2-1, mabao
yake yakifungwa na Magola Mapanda dakika ya 18 na Mutombo Kazadi dakika ya 67,
wakati la kufutia machozi la timu ya jeshi la Rwanda, lilifungwa na Jean
Mugiraneza dakika ya 89.
0 comments:
Post a Comment