Tetesi za J'tatu magazeti ya Ulaya
SPURS SASA KAZI IPO KUMPATA HUGO
KLABU ya Tottenham inakabiliwa na ugumu katika kuinasa saini ya kipa wa Lyon, Hugo Lloris kutokana na klabu hiyo ya Ufaransa kusema hawatamruhusu kuondoka hadi yeye mwenyewe aombe kuondoka.
KLABU ya Sunderland imeweka dau la pauni Milioni 12 kwa ajili ya mshambuliaji wa Wolves, Steve Fletcher, ambaye klabu hiyo ya Midlands inaamini ana thamani ya pauni Milioni 15.
Arsenal inaweza kusajili nyota mwingine kutoka ilipowatoa Theo Walcott na Alex Oxlade-Chamberlain, Southampton safari hii wakitaka kumsajili kinda wa miaka 17, beki wa pembeni, Luke Shaw.
CARROLL SASA HANG'OKI LIVERPOOL
KOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema kwamba Andy Carroll anaweza "kuingia kwenye mfumo wanaotaka kutumia" na kwamba mshambuliaji huyo anajisikia furaha kubaki kwa Wekundu wa Anfield.
KLABU ya Manchester City imemrudisha Nahodha wake Vincent Kompany England mapema kutoka kwenye ziara ya Mashariki ya mbali, hivyo beki huyo wa kati anaweza kupata tiba ya maumivu yanayomsumbua na kuwa fiti kwa mwanzo wa msimu.
KOCHA wa Tottenham, Andre Villas-Boas hakufurahia teke alilopigwa mchezaji wake Gareth Bale na mchezaji wa Liverpool, Charlie Adam katika iliyozikutanisha timu hizo na kumalizika kwa sare ya bila kufungana Marekani.
0 comments:
Post a Comment