// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ARSENAL YATAJA KIKOSI CHA KUWANIA KOMBE LA KWANZA 2012 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ARSENAL YATAJA KIKOSI CHA KUWANIA KOMBE LA KWANZA 2012 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, July 16, 2012

    ARSENAL YATAJA KIKOSI CHA KUWANIA KOMBE LA KWANZA 2012


    MARKUS LIEBHERR MEMORIAL CUP
    Johan Djourou anatarajiwa kucheza Southampton

    Ni fursa ya kushuhudia vipaji vipya ndani ya Arsenal

    KLABU ya Arsenal inaanza rasmi programu ya maandalizi ya msimu mpya Jumamosi kwa kugombea Kombe la kumbukumbu ya Markus Liebherr na itatumia mseto wa wachezaji vijana na wakongwe mjini Southampton.

    Kwa mujibu wa tovuti ya klabu hiyo, Washika Bunduki hao watamenyana na timu hiyo mpya katika Ligi Kuu, Southampton na Anderlecht ya Ubelgiji. Kikosi cha Arsene Wenger kitafungua nat Anderlecht saa 12.45 kwa saa za London, kabla ya kumenyana na wenyeji saa 2:00 kwa saa za huko.

    Arsene Wenger ametaja kikosi cha vijana kitakachoshuka kwenye Uwanja wa St Mary, wakiwemo na wazoefu kama GervinhoJohan DjourouMarouane ChamakhAndre SantosFrancis Coquelin na Kieran Gibbs katika kikosi cha wachezaji 23.

    Hakuna hata mchezaji mmoja wa Arsenal aliyecheza Euro 2012 aliyejumuishwa kwenye kikosi hicho, kwa sababu bado hawajaanza mazoezi.

    Lakini mashabiki wote wa Arsenal watakaohudhuria michuano hiyo watapata fursa ya kuwashuhudia Kyle BartleyVito Mannone na Henri Lansbury wakiwa na jezi za Arsenal tena, baada ya kufanya vizuri walipokuwa wakicheza kwa mkopo Rangers, Hull City na West Ham msimu uliopita.

    Pia watapata fursa ya kushuhudia vipaji vipya vya nyota wanaoinukia klabuni kama kiungo Mholanzi, Kyle Ebecilio, kinda lenye kipaji cha ajabu kutoka Sweden, Kristoffer Olsson nyota wa Ujerumani, Thomas Eisfeld.

    Kumbuka unaweza kufuatilia moja kwa moja michuano hiyo kupitia @Arsenal Twitter account. Tumia hashtag ya #AFCvAND kupata mechi na Anderlecht game na #SFCvAFC kupata mechi na Southampton.

    Taarifa za mechi pia zitapatikana katika tovuti ya klabu, Arsenal.com.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ARSENAL YATAJA KIKOSI CHA KUWANIA KOMBE LA KWANZA 2012 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top