MAHADHI MPYA; Kipa wa Mafunzo, Halid Mahadhi Haji akidaka mpira mbele ya mshambuliaji wa Yanga, Said Bahanuzi |
Yanga |
Mafunzo |
YANGA imefuzu kuingia Nusu Fainali ya Klabu Bingwa ya soka
Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, baada ya kuifunga Mafunzo ya
Zanzibar kwa penalti 5-3, kufuatia sare bya 1-1 ndani ya dakika 90 Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam, wawakilishi wa Zanzibar Mafunzo walikuwa wa kwanza kupata
bao lililofungwa na Ali Othman Mmanga, dakika ya 34, akiunganisha kona ya Juma
Othman Mmanga na Yangab wakasawazisha dakika ya 46, mfungaji Said Bahanuzi ‘Spider
Man’.
Yanga sasa itamenyana na APR ya Rwanda, keshokutwa
ambayo katika Robo Fainali ya kwanza, imeitoa URA ya Uganda kwa kuifunga 2-1,
mabao yake yakifungwa na Jean Claude Iranzi dakika ya tisa na Suleiman Ndikumana
dakika ya 34, wakati la Watoza Ushuru wa Kampala, lilifungwa na Robert Ssentongo
dakika ya 57.
Yanga SC; Yaw Berko, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Stefano Mwasyika, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na Rashid Gumbo.
Yanga SC; Yaw Berko, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Stefano Mwasyika, Haruna Niyonzima, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na Rashid Gumbo.
Benchi; Ally Mustafa ‘Barthez’, Shamte Ally, Ladislaus Mbogo, Godfrey
Taita, Juma Seif ‘Kijiko’, Jerry Tegete na Idrisa Rashid.
Mafunzo; Khalid Mahadhi Hajji, Ismail Khamis Amour, Said Mussa
Shaaban, Salum Said Shebe, Ali Othman Mmanga, Juma Othman Mmanga, Suleiman
Kassim ‘Selembe’, Jaku Juma Jaku, Mohamed Abdulrahim, Wahid Ibrahim na Ally Juma
Hassan.
Benchi; Salum Mohamed Pangani, Hajji Abdi Hassan, Kheir Salum
Kheir, Sadik Habib Rajab na Thabit
Mohamed Abdallah.
MECHI YA KWANZA....
Wachezaji wa APR wakimpongeza Ndikumana, aliyeinua vidole juu kushoto kwa kufunga bao la pili |
Dan Wagaluka wa URA kushoto akitafuta mbinu za kumtoka beki wa APR kulia |
0 comments:
Post a Comment