// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ZAWADI YA FATHER KIDEVU KWA WANANDOA MFANO WA KUIGWA TEDDY NA NESTOR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ZAWADI YA FATHER KIDEVU KWA WANANDOA MFANO WA KUIGWA TEDDY NA NESTOR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, June 28, 2012

    ZAWADI YA FATHER KIDEVU KWA WANANDOA MFANO WA KUIGWA TEDDY NA NESTOR


    "There is no more lovely, friendly and charming relationship, communion or company than a good marriage".

    KUMI NA TANO SI HABA (PONGEZI)
    Pongezi nina zituma, kwako Tedi nawe Nesto
    Mu imara kama chuma, kwa upendo wake Kristo
    Mungu awape uzima, mkalea na watoto,
    Kumi na tano si haba, Mroki nawapongeza.

    Mroki nawapongeza, kumi na tano si haba,
    Nesto leo umeweza, nyumbani waitwa baba,
    Tedi  ye hakuteleza, tuli yeye hakuyumba,
    Kumi na tano si haba, Kidevu nawapongeza.

    Mungu kawabariki, wana weri kawapa,
    Japo home hamshikiki, ulizi wana huwapa,
    Ibada mnashiriki, pongezi mi ninawapa,
    Kumi na tano si haba, Kidevu nawapongeza.

    Kubwa shukrani kwa mola, mja wetu wa karima,
    Alo ziepusha hila, kwetu sisi maamuma,
    Tedi waivaa shela, hakupenda dada wema,
    Kumi na tano si haba, Kidevu nawapongeza.

    Jala wetu wa Jalalu, wape zaidi hekima,
    Mmoja asiwe lulu, mwingini akawa Kima,
    Hapo hawatafaulu, kuheshimiana daima,
    Kumi na tano si haba, Kidevu nawapongeza.

    Wote mkajidhatiti, kwenye wenu upendo,
    Mkipiga Serengeti, msipigane mabindo,
    Kuweni watu wa geti, upole uwe mtindo,
    Kumi na tano si haba, Kidevu nawapongeza.

    Hizi saba zinatosha, kiu kimenikamata,
    Sio vyema kuwachosha, maneno mmeyapata,
    Nami nitajibidisha, yenu siri kuipata,
    Kumi na tano si haba, Kidevu nawapongeza.

    Mroki Mroki “Father Kidevu
    +255 717 002303

    -- 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ZAWADI YA FATHER KIDEVU KWA WANANDOA MFANO WA KUIGWA TEDDY NA NESTOR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top