Xavi |
KIUNGO wa Hispania, Xavi amevunja rekodi ya kugawa pasi
katika Kombe la Mataifa ya Ulaya usiku huu, akiiongoza timu yake kushinda 4-0 dhidi
ya Jamhuri ya Ireland.
Kiungo huyo mchezeshaji alitoa mapande 136 usiku wa Alhamisi
na kati ya hizo pasi 127 zilifika kwa walengwa. Rekodi ya awali ya pasi 117 iliwekwa
na gwiji wa Uholanzi, Ronald Koeman, ambaye alifanya mavitu hayo katika michuano
ya mwaka 1992 dhidi Denmark.
Hispania pia iliweka rekodi katika michuano ya Ulaya,
kutokana na kugonga pasi 860 dhidi ya Vijana wa Kijani.
La Roja walikisambaratisha kikosi cha Giovanni Trapattoni 4-0
huku wakitawala mchezo kwa asilimia 78.
Sasa wanaongoza Kundi C sambamba na Croatia, ambao watamenyana
nao katika mechi ya mwisho ya kundi hilo Jumatatu.
0 comments:
Post a Comment