• HABARI MPYA

        Monday, June 25, 2012

        WIMBLEDON TENISI YA 121 YAANZA LEO


        25 Juni, 2012 - Saa 12:12 GMT
        Li Na
        Li Na aliondolewa mapema katika French Open lakini anatazamiwa kufanya vyema katika mapambano ya Wimbledon

        MASHINDANO ya tenisi ya Wimbledon nchini Uingereza yameanza leo Jumatatu, na kati ya wachezaji mahiri wanaoshiriki ni pamoja na Novak Djokovic kutoka Jamhuri ya Serbia, Maria Sharapova ambaye ni raia wa Urusi na Roger Federer kutoka Uswisi.
        Waingereza saba pia wanashiriki katika mashindano ya mwaka huu.
        Kati ya wachezaji ambao mambo yameanza kuwaendea vyema Jumatatu ni Mchina Li Na, ambaye moja kwa moja ameingia raundi ya pili ya mashindano, kwa kumuondoa Ksenia Pervak wa Kazakhstan 6-3, 6-1.
        Baada ya kuondolewa mapema katika mashindano ya French Open katika raundi ya nne, Li Na inaelekea ameongeza juhudi za kufanya vyema katika mapambano ya Wimbledon.
        Hata hivyo alionekana amemzidi nguvu Pervak, mwenye umri wa miaka 21, na alimuondoa haraka chini ya muda wa saa moja.
        Sasa Li Na atakutana na Sorana Cirstea kutoka Romania, au Mfaransa Pauline Parmentier, katika raundi ya pili.
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: WIMBLEDON TENISI YA 121 YAANZA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry