Washiriki Miss Dar Inter College, nani ataibuka mshindi leo? Twendeni tukashuhudie |
Na Princess Asia
Dina 'Dodo' |
HAYAWI hayawi, hatimaye yamekuwa- shindano la Miss Dar Inter
College 2012 linatarajiwa kufanyika leo kwenye ukumbi wa Makumbusho, katikati
ya Jiji karibu kabisa na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), likisindikizwa na
burudani ya Mfalme wa
Bongo Fleva, Nassib Abdul au Diamond Platinum.
Diamond ambaye imeelezwa leo atatinga na mkoko wake mpya wa
‘bei chafu’ alioununua hivi karibuni katika shoo hiyo, ili mashabiki wake waune
kwa macho yao makavu, amepania kufanya mambo baab kubwa leo Miss Dar Inter
College 2012.
Shindano hilo, litakaloshirikisha mabinti wenye upeo wa hali
ya juu kutokana na ukweli kwamba wanatoka vyuoni, mbali na burudani ya Mfalme
wa Bongo Fleva, Diamond Platinum, pia litapambwa na burudani ya bendi mpya ya
muziki wa dansi inayokuja juu hivi sasa, Skylight.
Diamond atatinga na mkoko huu leo; umewahi kuuona live? |
Mratibu wa shindano hilo Dina Ismail Mkingiye ‘Dodo’,
ameiambia BIN ZUBEIRY maandalizi kwa ujumla yanaendelea vizuri na warembo
14 watakaoshiriki shindano hilo leo watafanyiwa usaili Dar es Salaam
“Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo
kutoka Miss Dar Inter College anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania,” alisema.
Warembo watakaoshiriki shindano hilo wanatoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na
Time, Ustawi wa Jamii, Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo Kikuu Huria (OUT) wakati taji la Miss
Inter College linashikiliwa na binti kutoka IFM, Rose Msuya.
Warembo wawili wa Inter College walishiriki fainali za Miss
Tanzania mwaka jana na kufanya vizuri, mbali na Rose mwingine ni mshindi wake
wa pili, Blessing Ngowi.
Dina aliyewahi kuandikia pia magazeti ya Majira, Spoti
Starehe na kutangazia Radio Times, aliwataja warembo wanaoshiriki shindano hilo
kuwa ni Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael,
Veronica Yollla, Jacqueline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada
Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Amewataja wadhamini wa shindano hilo kuwa ni Redd’s Premium,
Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band, Lamada Hotel, Screen Masters, Makumbusho
ya Taifa, Mustafa Hassanali, Shear Illusions, Lamada Hotel, Grand Villa Hotel,
Clouds Media Group blog za Michuzi, Dina Ismail, BIN ZUBEIRY, Mtaa kwa
Mtaa na Full Shangwe.
Moja ya vitu watavayoonyesha jukwaani leo ni shoo hii; kwa nini ukose? |
0 comments:
Post a Comment