// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WABAGUZI POLAND NJE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WABAGUZI POLAND NJE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, June 17, 2012

    WABAGUZI POLAND NJE


    16 Juni, 2012 - Saa 21:29 GMT
    Jamhuri ya Czech
    Ushindi wa Czech umewaondoa wenyeji Poland

    NYOTA wa Jamhuri ya Czech, Petr Jiracek alifunga bao la pekee katika mechi ya uwanja wa Wroclaw dhidi ya wenyeji Poland siku ya Jumamosi, na kuwahuzunisha mashabiki wa nyumbani, wakati Jamhuri ya Czech ilipofuzu kuingia robo fainali za mashindano ya Euro 2012.
    Jamhuri ya Czech imefuzu katika kundi hilo, baada ya kuongoza kwa pointi 6.
    Jiracek, kiungo cha kati wa timu ya Wolfsburg ya Ujerumani, aliweza kuutambariza mpira wavuni katika sehemu ambayo kipa Przemyslaw Tyton hakuweza kuwa na matumaini kabisa ya kuufikia mpira, zikiwa zimesalia dakika 18 tu mechi hiyo kumalizika.
    Poland walianza mechi wakifahamu kwamba iwapo wangelipata ushindi katika mechi hiyo, basi wangeliweza, kwa mara ya kuwanza, kuwa miongoni mwa timu nane ambazo zingelisalia katika mashindano kushiriki katika mechi za robo fainali.
    Nahodha wa Poland Jakub Blaszczykowski, katika juhudi za dakika ya mwisho alikuwa nusra afunga bao la kusawazisha, lakini ulinzi wa Czech ulikuwa thabiti, na mpira kuondolewa kabla ya kuvuka msitari.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WABAGUZI POLAND NJE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top