Na Prince Akbar
KUANZIA saa 4:00 asubuhi ya leo, zoezi la usaili kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa klabu ya Yanga, uliopangwa kufanyika Julai 15, mwaka huu watakuwa wakifanyiwa usaili makao makuu ya klabu, makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwani.
KUANZIA saa 4:00 asubuhi ya leo, zoezi la usaili kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa klabu ya Yanga, uliopangwa kufanyika Julai 15, mwaka huu watakuwa wakifanyiwa usaili makao makuu ya klabu, makutano ya Mitaa ya Twiga na Jangwani.
Louis Sendeu, Ofisa Habari wa Yanga, ameiambia BIN
ZUBEIRY asubuhi hii kwamba zoezi hilo litaongozwa na Kamati ya
Uchaguzi, chini ya Mwenyekiti wake, Jaji John Mkwawa na wagombea wote
wanatakiwa kufika wao wenyewe.
Tayari Kamati hiyo ya Mkwawa, imemuengua mgombea Nafasi ya
Makamu Mwenyekiti, Ally Mayay Tembele, kwa sababu hakufika kusikiliza pingamizi dhidi
yake.
Kuenguliwa kwa Mayay, kunafanya nafasi ya Makamu Mwenyekiti
ibakiwe na watu watatu, ambao ni Ayoub Nyenzi, Yono Kevela na Clement Sanga na
wote watafanyiwa usaili leo.
Nafasi ya Uenyekiti wagombea ni Yussuf Mehboob Manj, John
Jambele, Edgar Chibura na Sarah Ramadhani.
Katika nafasi za Ujumbe ni Lameck Nyambaya, Ramadhani Mzimba
‘Kampira’, Mohamed Mbaraka, Ramadhani Said, Edgar Fongo, Beda Simba, Ahmad Gao,
Mussa Katabaro, George Manyama, Aaron Nyanda, Abdallah Bin Kleb, Omary Ndula,
Shaaban Katwila, Jumanne Mohamed Mwammenywa, Abdallah Mbaraka, Peter Haule,
Justin Baruti na Abdallah Sharia.
Awali, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu,
Mfanyabiashara Muzamil Katunzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Eliakhim
Masu walichukua fomu za kugombea Ujumbe lakini wakashindwa kurudisha, wakati
Isaac Chanzi pia hakurudisha fomu ya Makamu Mwenyekiti hivyo moja kwa moja hao
hawamo katika kinyang’anyiro.
Uchaguzi huo, unaokuja baada ya Wajumbe wengi wa Kamati ya
Utendaji katika uongozi uliokuwa madarakani, akiwemo Mwenyekiti Wakili Lloyd
Baharagu Nchunga na Makamu wake, Davis David Mosha kujiuzulu utafanyika Julai
15, mwaka huu Dar es Salaam.
Tayari Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), ilitoa onyo kwa wagombea ambao waliwasilisha vyeti
visivyostahili na kutaka wawasilishe vyeti vinavyotambulika kwa mujibu wa
taratibu za uchaguzi, ambavyo ni vyeti vya Baraza la Mitihani.
0 comments:
Post a Comment