Venus Williams akiaga baada ya kutolewa usiku huu |
KATIKA miaka 15 tangu apoteze mechi ya kwanza ya Wimbledon,
Venus Williams alitwaa mataji matano ta All England Club na kujitambulisha kama
mmoja wa wachezaji wakali wa tenisi kihistoria.
Tangu hapo, hakuwahi kufungwa tena mechi ya raundi ya kwanza
hadi leo.
Williams ametolewa katika raundi ya ufunguzi ya michuano ya Wimbledon
kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1997, akifungwa na Elena Vesnina kwa 6-1, 6-3. Yalikuwa
ni matokeo ya kwanza mabaya zaidi kwa Williams kwenye michuano hiyo na pia
ilikuwa mara ya nne kufungwa katika raundi ya kwanza katika Grand Slam.
0 comments:
Post a Comment