Nasri |
Na Baraka MBolembole
Samir Nasri, Hatem Be
Arfa na Karimu Benzema kwa pamoja walikuwa wakifahamika kama wachezaji bora na
wenye vipaji zaidi katika soka la Ufaransa miaka mitano iliyopita, kundi hili
la vijana wenye asili ya Kiafrika kila mmoja alitajwa kama Zinedine Zidane
‘mpya’ hiyo ni kutokana na vipaji vya wachezaji hao. Miaka mitano baada ya
kufananishwa na ‘Zizzou’ ‘Waarabu’ hao watatu kesho watakuwa na jukumu kubwa la
kuiongoza nchi yao ya ‘hiari’ Ufaransa katika michuano ya Euro 2012
inayoendelea katika nchi za Poland na Ukraine. Ufaransa ambayo iliifunga
wenyeji wwenza wa michuano hiyo Ukraine katika mchezo wa ijumaa iliyopita
imefufua matumaini ya kufuta ‘aibu’ ya miaka minne iliyopita waliposhindwa
kuvuka hatua ya makundi, sasa wana pointi nne sawa na England, lakini
wanaongoza kundi la mwisho kutokana na kuwa na wastani mzuri wa mabao ya
kufunga na kufungwa, baada ya sare dhidi ya England jumatatu hii ‘Les Blues’
walitumia nguvu ya ziada ili kuwafunga Ukraine ambao tayari walikuwa na pointi
tatu walizozipata katika mchezo wa kwanza dhidi ya Ireland ambayo tayari
imeondoshwa katika michuano hiyo.
Blanc. kocha wa Ufaransa |
Ufaransa ambayo haikuwa na matokeo mazuri kwa
takribani kipindi cha miaka kumi iliyopita, itakumbuka namna ilivyosota tangu
walipofikia kilele cha mwisho ya mafanikio yao kisoka baada ya kuifunga Italia
mabao 2-1 katika fainali ya mwaka 2000. Baada ya kushuhudia kizazi cha dhahabu
kilichojumuhisha wachezaji wenye vipaji kama , Zidane, Cristopher Dugary, Youry
Jorkaeff, Emma Petit, Patric Vieirra, Thieery Hennry, David Trezeguet, Macel
Dessailly, Laurent Blanc ambaye ndiye kocha wa sasa wa timu hiyo, Bixente
Lizarrazu, Frank Rebouf, Fabien Barthez, aliyekuwa nahodha Didier Deschamps na
wengine kikimaliza kwa mafanikio, timu hiyo maarufu kama ‘Les Blues’ ilikwenda
katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2002 na kuutema ubingwa waliokuwa
wametwaa miaka minne nyuma (1998), siyo tu kuutema ubingwa, Ufaransa ilitolewa
katika michuano ile pasipo kufunga bao lolote, na baada ya kuifunga England
katika mchezo wa ufungi wa michuano ya Euro 2004, timu iliyokuwa na baadhi ya
wachezaji wake nyota walioipatia mafanikio katika miaka ya 1998, na 2000
walitolewa katika hatua ya robo fainali na waliokuja kuwa mabingwa Ugiriki, baada
ya kuzidiwa mbinu za kufunga na kuzuia kwa ushirikiano wa timu nzima, kasha
wakapata mafanikio ‘kiasi’ ya ‘kubahaitisha’ katika michuano ya kombe la dunia
mwaka 2006 nchi Ujerumani kabla ya kufungwa na Italia katika mchezo wa fainali
kwa mikwaju ya penalty. Wakashindwa kupata mafanikio katika michuano ya Euro
2008 kwa kushindwa kuvuka hatua ya makundi na kasha wakashindwa kuvuka tena
hatua ya makundi katika fainali za kombe la dunia nwaka 2010 baada ya kufuzu
‘kimagumashi’ kwa pasi ya mkono siku ya mchezo wa ‘play off’ dhidi ya Ireland.
Na sasa wanatakiwa kuifunga tena Ukraine ili waweze kuwa na uhakika wa kufuzu
kwa robo fainali baaada ya miaka nane.
Ufaransa yenye vijana
kama, Nasri, Benzema, Ben Arfa, Alou Diarra, Yoan Cabaye, Frank Ribery, Jerem
Menez ambaye alianza na kufunga bao katika mchezo uliopita, Mexes ambao kwa
pamoja walikuwa na msimu bora katika vilabu vyao wanaweza kufanya moja ya
‘maajabu’ kwa kutwaa ubingwa ‘kimiujiza’ siku ya mwisho ya michuano endapo
watakuwa watulivu na kuwa makini na kile ambacho kimewapeleka uko. Ufaransa
katika kipindi cha miaka kumi iliyopita imekuwa na matatizo mengi katika kambi
yao hasa kipindi wakiwa katika michuano mikubwa. Kama timu itatulia na
wachezaji wakafanya kazi bila shaka lolote wanaweza kufanya, kufika nusu
fainali yatakuwa ni mafanikio makubwa kwao lakini wanaweza kucheza fainali pia
na kutwaa taji kwani nao ni wazoefu wa michezo ya hatua ya mtoano, walitwaa
kombe la dunia mwaka 1998 baada kujilinda na mabeki kufunga mabao muhimu, na
kwenye Euro 2000 ilikuwa ni hivyo hivyo, lakini baada ya hapo matatizo ya utovu
wa nidhamu kwa wachezaji muhimu wa safu ya ulinzi yamewaangusha na kuwafikisha
hapo walipo sasa, lakini hivi sasa wakiwa na mchezaji ambaye Wafaransa
wanamuona no bora zaidi katika safu ya ulinzi ya timu yao, Phillipe Mexex na
uwepo wa walinzi ‘viongozi’ kama Patrice Evra na Gael Clichy bila shaka timu
hii inahitaji nidhamu tu kabla ya kufanya ‘maajabu’ ya mchezo wa soka. Bila
shaka huenda wengi wasiipe nafasi kubwa ya kutamba katika michuano hii, lakini
ni timu ambayo inaweza kucheza nusu fainali, fainali na hata kutwaa taji, mara
kadhaa wameweza kufanya hivyo. Je wataweza tena safari hii? Mimi utabiri wangu
ni huu, bingwa anaweza kuwa Ujerumani, Italia au Hispania.
0714 08 43 08 / 0688 54 59 92
0 comments:
Post a Comment