// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); UEFA WAIADHIBU CROATIA KWA KULIANZISHA EURO 2012 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE UEFA WAIADHIBU CROATIA KWA KULIANZISHA EURO 2012 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, June 16, 2012

    UEFA WAIADHIBU CROATIA KWA KULIANZISHA EURO 2012


    16 Juni, 2012 - Saa 12:47 GMT
    Italia na Croatia
    Italia na Croatia

    SHIRIKISHO la Soka Ulaya, (UEFA), limeitoza faini ya Euro 25,000 Chama cha Soka Croatia kwa ghasia zilizozushwa na mashabiki wake wakati wa pambano kati ya timu yao na Jamhuri ya Ireland.
    Mashabiki wa Croatia walirusha fashfash wakati wa mechi hio mjini Poznan iliyomalizika kwa ushindi wa 3-1 jumapili iliyopita.
    Mashabiki wa Croatia
    Mashabiki wa Croatia
    Wahudumu wa uwanja walikabiliana na mashabiki waliovunja uzio na moja kwa moja kwenda kumbusu Kocha wa Timu ya Taifa Slaven Bilic.
    "hukumu hii imechukuliwa kwa sababu mashabiki waliasha moto na kurusha fashifashi na mizinga pamoja na kuvamia uwanja,imesema taarifa ya Uefa.
    Wakati huo huo Uefa inachunguza madai kwamba ndizi ilirushwa uwanjani wakati wa mechi ya kundi C kati ya Italia na Croatia siku ya Alhamisi.
    Mpiga picha mmoja alishuhudia wahudumu wa uwanja wakiokota ndizi na kusikia miliyo ya nyani iliyoelekezwa mshambuliaji wa Italia Mario Balotelli.
    Croatia itapambana na bingwa wa Dunia na pia wa Ulaya Uhispania katika mechi ya mwisho ya makundi siku ya jumatatu mjini Gdansk.
    Ushindi au sare ya 2-2 itaiwezesha Croatia kusonga mbele kujiunga na Timu nane zilizovuka hatua ya makundi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UEFA WAIADHIBU CROATIA KWA KULIANZISHA EURO 2012 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top