Na Prince Akbar
MABINGWA wa soka Afrika Mashariki na Kati, Yanga SC leo
wanashuka dimbani kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kumenyana na mabingwa
wa Uganda, Express ‘Red Eagles’ katika mchezo wa kirafiki, wenye lengo la
kuwatambulisha wachezaji wake.
Ofisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu ameiambia BIN
ZUBEIRY maandalizi yote ya mchezo huo yamekamilika na amewataka wapenzi
wa Yanga kumiminika kwa wingi uwanjani kuwaona wachezaji wao wapya.
Sendeu amesema kwamba wachezaji wote wapya wa Yanga watapewa
nafasi leo, ili kuanza kuzoeana na mashabiki wa klabu hiyo.
Miongoni mwa wachezaji wapya wa Yanga, wanaotarajiwa kuwa
kivutio leo ni kipa Ally Mustafa Mtinge ‘Barthez’, beki Kelvin Yondan wote
kutoka Simba, beki Juma Abdul kutoka Mtibwa Sugar, beki Ladislasu Mbogo kutoka
Toto African, viungo Nizar Khalfan aliyekuwa anacheza Marekani, Frank Damayo
kutoka JKT Ruvu, washambuliaji Said Bahanuzi ‘Ortega’ kutoka Mtibwa Sugar na
Ally Msuva kutoka Moro United.
Lakini pia bado wachezaji wa zamani wa klabu
hiyo, kama Hamisi Kiiza, Haruna Niyonzima, Rashid Gumbo, Jerry Tegete, Nadir
Haroub ‘Cannavaro’ wataendelea kuwa kivutio katika klabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment