Dina Ismail Mkingiye 'Dodo', Mratibu Miss Dar Inter College |
Na Princess Asia
VIMWANA wanaotarajiwa kushiriki shindano la Miss Dar Inter College
2012 litakalofanyika Ijumaa wiki hii kwenye ukumbi wa Makumbusho, katikati ya
Jiji karibu kabisa na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), kesho watajivinjari
katika ukumbi Club Billicanas, Dar es Salaam kupiga promo la shoo yao,
inayosubirwa kwa hamu na wapenzi wengi wa sanaa ya ulimbwende nchini.
Wanyange wa Miss Dar Inter College katika ukumbi wa Billz
kesho wamealikwa kwenye shoo ya Usiku wa wa Mwafrika ya bendi ya African Stars ‘Twanga
Pepeta’, ikiwa ni siku mbili kabla ya shindano lao linaloshirikisha mabinti kutoka
vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu Dar es Salaaam.
Shindano hilo, litakaloshirikisha mabinti wenye upeo wa hali
ya juu kutokana na ukweli kwamba wanatoka vyuoni, litapambwa na burudani ya
muziki kutoka kwa Mfalme wa Bongo Fleva, Nassib Abdul ‘Diamond Platinum’ pamoja
na bendi mpya ya muziki wa dansi inayokuja juu hivi sasa, Skylight.
Mratibu wa shindano hilo Dina Ismail Mkingiye ‘Dodo’,
ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba warembo wote wanaoshiriki shindano hilo,
watakuwepo kwenye shoo ya Twanga Pepeta usiku wa kesho.
Diamond Platinum atatumbuiza Ijumaa Makumbusho ya town |
Akizungumzia maandalizi ya shindano hilo, Dina ambaye ni
mwandishi mwandamizi wa habari za Michezo wa gazeti la Tanzania Daima, alisema yanaendelea
vizuri na warembo 14 watakaoshiriki shindano hilo wanaendelea na mazoezi katika
hoteli ya The Grand Villa, Kijitonyama, Dar es Salaam
“Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo
kutoka Miss Dar Inter College anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania,” alisema
mama huyo wa watoto watatu, P, Checha na Baito ambaye pia Mkurugenzi wa
dinaismail.blogspot.com ‘inayokimbiza ile mbaya’.
Warembo watakaoshiriki shindano hilo wanatoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na
Time, Ustawi wa Jamii, Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo Kikuu Huria (OUT) wakati taji la Miss
Inter College linashikiliwa na binti kutoka IFM, Rose Msuya.
Warembo wawili wa Inter College walishiriki fainali za Miss
Tanzania mwaka jana na kufanya vizuri, mbali na Rose mwingine ni mshindi wake wa
pili, Blessing Ngowi.
Dina aliyewahi kuandikia pia magazeti ya Majira, Spoti
Starehe na kutangazia Radio Times, aliwataja warembo wanaoshiriki shindano hilo
kuwa ni Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael,
Veronica Yollla, Jacqueline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada
Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Amewataja wadhamini wa shindano hilo kuwa ni Redd’s Premium,
Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band, Lamada Hotel, Screen Masters, Makumbusho
ya Taifa, Mustafa Hassanali, Shear Illusions, Lamada Hotel, Grand Villa Hotel, Clouds
Media Group blog za Michuzi, Dina Ismail, BIN ZUBEIRY, Mtaa kwa Mtaa na Full Shangwe.
Baadhi ya washiriki Miss Dar Inter College wakiwa mazoezini |
0 comments:
Post a Comment