TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania imetolewa katika kinyang'anyiro cha kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani Afrika Kusini, baada ya kufungwa kwa penalti 7-6 kufuatia sare ya 1-1.
Timu zilipokwenda kwenye mikwaju ya penalti, Stars ilifungwa 7-6. Mechi ya kwanza timu hizo zilitoka 1-1 pia. Katika mchezo huo, Msumbiji walitangulia kupata bao na katika dakika za majeruhi Aggrey Morris akaisawazishia Stars.
Timu zilipokwenda kwenye mikwaju ya penalti, Stars ilifungwa 7-6. Mechi ya kwanza timu hizo zilitoka 1-1 pia. Katika mchezo huo, Msumbiji walitangulia kupata bao na katika dakika za majeruhi Aggrey Morris akaisawazishia Stars.
Refa Bennett Daniel alipopuliza filimbi ya kumaliza dakika 90 za pambano hilo timu hizo zilikuwa zimefungana bao 1-1, hivyo kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo yanayoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) mikwaju ya penalti ikatumika kupata mshindi.
Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Dar es Salaam, Februari 29 mwaka huu timu hizo
zilitoka sare ya bao 1-1.
Msumbiji ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 9 lililofungwa na mshambuliaji Jeremias Sitoe akiungnisha krosi ya Elias Pelembe ambaye mabeki wa Taifa Stars walifikiri ameotea.
Stars ilisawazisha bao hilo dakika ya 89 likifungwa kwa kichwa na Aggrey Morris kutokana na mpira wa kona uliopigwa Amir Maftah.
Mikwaju ya penalti tano tano walioifungia Stars walikuwa Amir Maftah, Shabani Nditi na Shomari Kapombe wakati Aggrey Morris na Kevin Yondani walikosa.
Kwa vile The Mambas nao walikosa mbili ikabidi iongezwe penalti moja moja. Waliofunga kwa upande wa Stars walikuwa John Bocco, Frank Domayo na Mrisho Ngassa wakati Mbwana Samata alikosa.
Akizungumzia pambano hilo, Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen aliwapongeza wachezaji wake kwa kupambana hadi dakika ya mwisho.
"Tulikuja Maputo tukijua kuwa tunatakiwa kufunga bao, tumeweza kufunga bao ingawa katika dakika za mwisho. Unajua linapokuwa suala la penalti chochote kinaweza kutokea, na ndivyo ilivyokuwa," alisema Kim.
Taifa Stars itarejea nyumbani Juni 19 mwaka huu, ambapo itaaondoka hapa saa 4.40 asubuhi kwa kupitia Nairobi, Kenya na kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 1.50 usiku.
Kikosi kilipngwa hivi; Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni/John Bocco, Aggrey Morris, Kevin Yondani, Shaabani Nditi, Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Thomas Ulimwengu/Haruna Moshi, Mbwana Samata na Mwinyi Kazimoto/Amir Maftah.
0 comments:
Post a Comment