Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholaus Musonye kulia akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi za TFF, mchana huu. Kushoto ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah. |
Na Prince Akbar
MABINGWA watetezi wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati,
Kombe la Kagame watafungua dimba na Atletico ya Burundi katika mchezo wa Kundi
C wa michuano hiyo, Julai 14, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wakati
wapinzani wao wa jadi, Simba SC waliowekwa Kundi A, wataanza na URA ya Uganda
Julai 16, kwenye Uwanja huo huo.
Wawakilishi wengine wa Tanzania katika michuano hiyo, Azam
FC wao wataanza na Mafunzo ya Zanzibar katika mchezo wa Kundi B, Uwanja wa
Chamazi, Julai 15.
Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati
(CECAFA), Nicholaus Musonye amesema katika Mkutano na Waandishi wa Habari
mchana huu, ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ilala, Dar es Salaam
kwamba, Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) itashiriki kama
timu mualikwa.
Aidha, habari za kusikitisha ni kwamba, Musonye amesema Sudan,
Ethiopia, Eritrea na Somalia hazitaleta wawakilishi wao kwa sababu mbalimbali.
Wakati Ethiopia ligi yao inaanza wiki hii, Sudan wawakilishi
wao wapo kwenye michuano ya Afrika na wameshindwa kuteua timu mbadala, Somalia
wawakilishi wao Elman wamebadilisha uongozi, hivyo bado hawajajipanga na
Eritrea kutokana na desturi ya wachezaji wao kuzamia kila wanapokuja kwenye
mashindano, wameondolewa.
“Wameondolewa, kwa sababu mbili, kwanza nchi yao imeomba
ipewe muda kulifanyia kazi sual hilo, na sisi pia (CECAFA) tunalitafutia
ufumbuzi,”alisema Musonye.
Lakini Musonye amekiri kitendo cha kuyatoa mashindano hayo
mwanzoni mwa mwaka hadi katikati ya mwaka kumechangia baadhi ya timu
kutoshiriki na amesema tayari amewasilisha pendekezo kwenye Mkutano Mkuu, mashindano
yarejee kufanyika mwanzoni mwa mwaka kama ilivyokuwa awali.
Kuhusu mechi ya ufunguzi ya Simba kuchezwa Julai 16, ambayo
itakuwa Jumatatu badala ya Jumapili, Musonye alisema kwamba imetokana na kwamba
Julai 15, Uwanja wa Taifa kutakuwa na fainali za Copa Coca Cola, ambayo maandalizi
yake yote yamekamilika.
Yanga ndiye bingwa mtetezi wa mashindano, baada ya kuifunga
Simba SC katika fainali mwaka jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
CECAFA CLUB KAGAME CUP 2012
14th – 28th July 2012, Dar-Es Salaam, Tanzania
Team Fixture list
GROUP A SIMBA(TZ), URA (UGA), VITA CLUB (CONGO DR) PORTS (DJB),
GROUP B AZAM(TZ), MAFUNZO(ZANZ), TUSKER (KEN),
GROUP C YANGA(TZ), APR(RWD),WAU SALAAM (SOUTH SUDAN), ATLETICO(BUR),
(QUALIFICATION: GROUP A 1st and 2nd AND 3rd GROUP B 1st and 2nd , GROUP C 1st and 2nd AND 3rd QUALIFY TO QUARTER FINALS).
DATE
|
NO
|
TEAMS
|
GROUP
|
VENUE
|
TIME (EAT)
| ||
Sat 14th July
|
1
2
|
APR Vs WAU SALAAM
YANGA v ATLETICO
|
C
C
|
Dar
Dar
|
2pm
4 PM
| ||
Sun 15THJuly
|
3
|
AZAM V MAFUNZO
|
B
|
CHIMANZI
|
4 PM
| ||
Mon 16th July
|
4
5
|
VITA CLUB Vs PORTS
SIMBA Vs URA
|
A
A
|
Dar
Dar
|
2PM
4PM
| ||
Tue 17th July
|
6
7
|
ATLETICO Vs APR
WAU SALAAM Vs YANGA
|
C
C
|
Dar
Dar
|
2pm
4PM
| ||
Wed 18th July
|
8
9
|
VITA CLUB Vs URA
PORTS Vs SIMBA
|
A
A
|
Dar
Dar
|
2 pm
4pm
| ||
Thu 19th July
|
10
11
|
ATLETICO Vs WAU Salam
MAFUNZO Vs TUSKER
|
C
B
|
Dar
Dar
|
2pm
4pm
| ||
Fri 20th July
|
12
13
|
PORTS Vs URA
YANGA Vs APR
|
A
C
|
Dar
Dar
|
2pm
4pm
| ||
Sat 21st July
|
14
15
|
AZAM Vs TUSKER
SIMBA Vs VITA CLUB
|
B
A
|
TBD
TBD
TBD
TBD
|
TBD
| ||
Sun 22nd July
|
REST DAY
| ||||||
QUARTER FINALS
| |||||||
Mon 23th July
|
16
17
|
B2 Vs C2
A1 Vs C3
|
TBD
|
TBD
| |||
Tue 24th July
|
18
19
|
C1 Vs A2
B1 VsA3
|
TBD
|
TBD
| |||
Wed 25th July
|
REST DAY
| ||||||
SEMI FINALS
| |||||||
Thu 26th July
|
20
|
Winner 16 Vs Winner 17
|
TBD
|
TBD
| |||
Thu 26th July
|
21
|
Winner 18 Vs Winner 19
|
TBD
|
TBD
| |||
Fri 27th July
|
REST DAY
| ||||||
FINALS AND 3rd PLACE PLAY OFFS
| |||||||
Sat 28th July
|
22
23
|
Loser 20 Vs Loser 21
Winner 20 Vs Winner 21
|
TBD
|
TBD
|
0 comments:
Post a Comment