13 Juni, 2012 - Saa 18:39 GMT
Roberto Di Matteo
CHELSEA hatimaye imemteua Roberto Di Matteo kama meneja wake wa kudumu kwa kutiliana saini mkataba wa miaka miwili.
De Matteo aliipa Chelsea Kombe la FA na Ulaya
Di Matteo aliwekwa kama kocha wa mda kufuatia kutimuliwa kwa Andre Villas-Boas mnamo mwezi Machi, na akaweza kuiongoza klabu hio akifanikiwa kuifikisha na kushinda fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na vilevile kombe la FA la England.
Meneja huyo aliyekua kiongozi wa MK Dons na pia West Brom, Di Matteo alipoteza mechi tatu tu kati ya mechi 21 alizosimamia, na kutokana na hali hiyo wachezaji wengi wa klabu waliunga mkono ateuliwe kama meneja wa kudumu hususan baada ya kushinda kombe lililoikwepa klabu hio kwa mda mrefu la Mabingwa wa Ulaya.
UEFA YALAANI VURUGU EURO 2012
13 Juni, 2012 - Saa 14:24 GMT
Mashabiki wazipiga
SHIRIKISHO la soka barani Ulaya, UEFA limeshutumu ghasia zilizotokea kwenye mitaa ya mji wa Warsaw kabla ya pambano la jumanne kati ya mwenyeji mshirika wa mashindano ya Euro2012 Poland na Urussi.
Polisi imewatia mbaroni watu 184,ikiwa ni raia 156 wa Poland na Warussi 24 kufuatia mapigano makali baina ya mashabiki ambao waliwashambulia Polisi pia.
Wakuu wa nchi walikua wamejiandaa kwa uwezekano wa mtafaruku kutokea kabla ya mchuano wa jumanne ikizingatiwa kwamba uhusiano kati ya nchi hizi mbili umetiwa sumu na migogoro ya miaka mingi ikikumbukwa pia uvamizi na utekaji wa Poland kwa kipindi cha miaka 40 baada ya vita vikuu vya pili vya Dunia.
Ghasia zilizuka wakati maelfu ya mashabiki wa Urussi wakisindikizwa na polisi walivuka mto Vistula wakiwa njiani kwenda uwanjani. Mapigano mengine yalizuka katikati ya mji katika eneo la mashabiki baada ya mechi iliyomalizika kwa sare ya bao moja kwa kila upande.
Waliopigana wakamatwa
Waliokamatwa watahukumiwa na mamlaka inayohusika.
Mbali na matukio ya nje ya uwanja, mechi iliendelea bila tatizo ndanio ya uwanja bila kubaguana. Kinyume na ilivyo katika mechi za Ligi nyingi barani Ulaya safari hii hapakuepo wasimamizi kulinda usalama kwa kusimama katikati ya makundi ya mashabiki wanaokinzana.
0 comments:
Post a Comment