Na Princess Asia
BAADA ya mafanikio makubwa ya kumleta mcheza sinema maarufu
wa Marekani Deidre Lorenz kushiriki mbio za Mount Kilimanjaro Marathon
zilizotimua vumbi tarehe 24 Juni 2012 sasa klabu ya Mout Kilimanjaro Marathon
1991 imeanzisha mbio za “Great Kilimanjaro Run – GKR”
GKR zitafanyika mjini Moshi kila mwaka kuanzia tarehe 22 -
28 October 2012 zikishirikisha klabu zote za riadha kutoka mkoa wa Kili
manjaro. GKR itazishikisha mbio fupi (Track and Field events) na kumalizia na
marathon siku ya jumapili tarehe 28 October.
Akizungunzia uamuzi wa kushirikisha mbio fupi katika GKR
Rais wa klabu ya Mt. Kilimanbjaro Marathon 1991 Onesmo Ngowi alisema kuwa klabu
yake inataka kuziendeleza pia mbio fupi na michezo mingine ya uwanjani badala
ya kuweka juhudi zote kwenye marathon tu.“Watu wamekazania sana marathon na
kusahau mbio fupi ambazo zilishawahi kuliletea taifa hili sfa kubwa sana”
alisema Ngowi kwa msisitizo.
Kuanzishwa kwa GKR kutaufanya mji wa Moshi kuwa na mbio tatu
za marathon kwa sasa na hii inaufanya mji huu kutoa nafasi kubwa kwa wanariadha
kukuza na kuendeleza vipaji vyao.
Tutamleta Haile Gabreselasie aje kuzindua mbio hizi” alisema
Ngowi ambaye mwaka jana alikuwa na mazungumzo marefu jijini Addis Ababa na
gwiji hili la mbio ndefu duniani kutoka nchi ya Ethiopia. Ngoiwi aliweza pia
kutiliana mkataba na shirika la ndege la Ethiopia (Ethiopia Airlines) jijini
Addis Ababa kufadhili mbio za Mount Kilimanjaro Marathon. Kwa sasa Ethiopia
Airlines (ET) ndio wafadhali pekee wa Mount Kilimanjaro Marathon. ET wanatoa
punguzo kwa wakimbiaji wanaoshirtiki kwenye mbio hizi kutoka sehemu mbalimbai
duniani.
Aidha, ET wanalipia gharama za kutangaza mbio hizi wakati wa
New York Marathon, L.A Marathon na Boston Marathon. Hii inaitangaza sana
Tanzania kwani mbio hizi tatu zinawashirikisha wakimbiaji wengi sana kutoka
katika nchi nyingi duniani. Kwenye mbio hizi za Marakani Mt. Kilimanjaro
Marathon huweka banda la maonyesho linaloitangaza Tanzania na vivutio vyake.
Pia Mt. Kilimanjaro Marathom huchezesha nahati nasibu
(raffle) kwenye mbio hizi tatu za Marekani ili kuwapata washiriki maarufu kama
Deidre Lorenz kuja kukimbia na kuitangaza vyema Tanzania.
Aliendelea kusema kuwa nchi hii ni yetu sote hivyo tuna
jukumu la kuitangaza na kuiendeleza wote alisisitiza Ngowi ambaye mwaka 2000
ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilimpa tuzo ya
“Mwanateknolojia wa Karne ya 20” kwa juhudi zake za kuendeleza Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Ngowi anawaalika watu binafsi, makampuni na taasisi
kushirikiana naye kuendeleza Utalii wa michezo hapa Tanzania ili kuipeleka nchi
hii hatua moja mbele kwenye utandawazi. Kwa wale wanaotaka kuwasiliana naye
kuhusu ufadhili watumie anwani ya barua pepe yangowio@yahoo.com au wapige simu
namba 0754-360828.
0 comments:
Post a Comment