// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PREVIEW STARS V MAMBAS; VIJANA LAZIMA WASHINDE LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PREVIEW STARS V MAMBAS; VIJANA LAZIMA WASHINDE LEO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, June 17, 2012

    PREVIEW STARS V MAMBAS; VIJANA LAZIMA WASHINDE LEO


    Kikosi cha Stars kilichoiua Gambia Jumapili Taifa.

    Na Prince Akbar
    TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo ina kibarua kigumu mjini Maputo, Msumbiji wakati itakapokuwa ikimenyana na wenyeji, Mambas katika mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani nchini Afrika Kusini.
    Taifa Stars, ambayo kwenye mechi ya kwanza ililazimishwa sare ya 1-1 mjini Dar es Salaam, inatakiwa lazima kushinda au japo ikikwama kabisa itoe sare ya mabao yasiyopungua 2-2 au zaidi.
    Taifa Stars inaonekana kuimarika kwa sasa na si sawa na ile iliyomenyana na Mambas Febrauri 29, mwaka huu na kutoka sare ya 1-1.
    Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY asubuhi ya leo kutoka Maputo kwamba, tayari Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulen ametaja kikosi chake kitakachoanza mechi ya leo na katika safu ya ushambuliaji amewapanga pamoja washambuliaji wa Tout Puissant Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu.
    Katika mechi hiyo itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa ulioko Zimpeto nje kidogo ya Jiji la Maputo kuanzia saa 9:00 kamili kwa saa za huko sawa na saa 10:00 kwa saa za kwetu, Poulsen amemuacha benchi beki Amir Maftah na atamuanzisha Erasto Nyoni katika beki ya kushoto.
    Safu ya ulinzi ya Stars itaongozwa na mlinda mlango na Nahodha wa timu hiyo,
    Juma Kaseja, wakati Shomari Kapombe atacheza beki ya kulia, kushoto Erasto Nyoni, waakti katikati watasimama Mwanasoka Bora wa Tanzania, Aggrey Morris na Kelvin Yondani.
    Ameweka viungo wakabaji wawili, Shaabani Nditi atakayecheza chini na Frank Damayo atakayecheza juu wakati huo huo Mwinyi Kazimoto atacheza kushoto na Mrisho Ngassa kulia, wakati washambuliaji ni Ulimwengu na Samatta.
    Maana yake leo, kutokana umuhimu wa Stars kutoruhusu bao leo huku ikisaka mabao, Poulsen amemuweka Damayo na Nditi ili wakabe sana, wakati Mwinyi na Ngassa watakuwa na kazi ya upishi.
    Ulimwengu ana sifa ya kuwa nguvu na uwezo wa kukokota mpira, wakati Samatta anakimbiza na uwezo wa kuwatoka mabeki kwa chenga, kuwakokota na pia ni mjanja mno.
    Dhahiri Stars itatawala mchezo leo, kwa sababu Ngassa ana uwezo mkubwa wa kushambulia- hivyo ni sawa na kucheza na washambuliaji watatu wakati Mwinyi atakuwa akiwachezesha washambuliaji hao.
    Damayo na Nditi, wote pamoja na kuwa wakabaji, lakini pia ni watoaji wazuri wa pasi ndefu na fupi.
    Kama ilivyokuwa kwenye mechi na Gambia Jumapili iliyopita, kuna uwezekano kiungo ‘fundi’ Haruna Moshi ‘Boban’ akatokea benchi kipindi cha pili kwenda kuimarisha safu ya ushambuliaji na dhahiri atachukua nafasi ya Ulimwengu.  
    Stars ikishinda mechi ya leo, itapangwa kwenye Kundi kucheza  mtindo wa ligi kuwania tiketi ya kucheza fainali za AFCOn mwakani, ambazo zinakuja mapema ili kukwepa kugongana na Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014.
    Kila la heri Taifa Stars. Mungu ibariki Tanzania.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PREVIEW STARS V MAMBAS; VIJANA LAZIMA WASHINDE LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top