Deidre akizungumza na Waandishi wa habari |
Na Princess Asia
MCHEZA sinema maarufu wa Marekani Deidre Lorenz ameahidi
kuleta wacheza sinema wenzake na kushiriki kwenye mbio za mwaka kesho za mt.
Kilimanjaro Marathon zitakazokuwa zinatimiza miaka 23 tangu zianzishwe mwaka
1991.
Lorenz aliyekimbia mbio za mwaka huu ambazo zilipewa jina la
“mbio za kutimiza miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika” na Bodi ya Utalii Tanzania
(TTB) amesema kuwa atakuja na timu yake ya wapiga picha ili kupiga picha
vivutio kadhaa vya Tanzania ikiwa ni pamoja na mlima Kilimanjaro. Qwiji hili la
sinema za Santorini Blue, The Great Fight, Perfect Strangers na nyingine nyingi
ameelezea kuipenda sana Tanzania.
“Sikutegemea kuikuta nchi nzuri kama hii” alisema mcheza
sinema huyo ambaye ameshawahi kuchaguliwa zaidi ya mara 4 kugombea tuzo maarufu
za Oscar. “Sasa nimeamini kuwa mlima Kilimanjaro ni mali ya Tanzania na
nitautangaza katika sinema zangu zote”aliendelea kusema Deidre Lorenz.
Mcheza sinema huyu ambaye ameingia kwenye mkataba na kampuni
kubwa ya Google hivi karibuni ili kuuza sinema zake katika mtandao aliielezea
Tanzania kama nchi nzuri na yenye watu wakarimu sana.
Mbio za Mount Kilimanjaro Marathon zilianzishwa mwaka 1991
na Marie Frances anayetoka katika jiji la matajiri la Bethesda nchini Marekani
baada ya kuombwa na balozi wa zamani wa Tanzania nchini Misri. Tangu kuanzishwa
kwake mbio hizi zimekuwa zinaleta watalii matajiri katika mji wa Moshi kupanda
mlima Kilimanjaro na kukimbia mbio hizi zinazojulikana kama Seven Continental
Races.
Hakuna masharti yote ya kukimbia mbio hizi na watanzania
wanaoshiriki katika mbio hizi huwa hawatozwi pesa za kiingilio.
Kwa kutambua mchango wake katika uchumi wake Manispaa ya
Moshi iliibadilisha jina barabara ya zamani ya Bustani Ale na kuiita Marie
Frances Boulevard ili kumuenzi mama huyu aliyejitolea maisha yake kuutangaza
mlima Kilimanjaro.
“Kila siku napokea ujumbe kutoka nchi mbalimbali niende huko
kuanzisha mbio za marathon lakini kwa sasa basi” alisema mama huyo aliyekuwa
mtayarishaji wa vipindi vya televisheni ya ABC kabla ya kunzisha Mt.
Kilimanjaro Marathon.
Alisema kuwa mwaka jana yeye na Rais wa klabu ya Mt.
Kilimanjaro Marathon mtanzania Onesmo Ngowi walifanya makubaliano ya Ethiopia
Airlines (ET) jijini Addis Ababa kuzifanya mbio hizo kuwa za kimataifa zaidi.
“ET walikubali kutoa ufadhili kwetu na pia kugharamia kushiriki kwetu katika
mbio za New York Marathon, Boston Marathon na Los Angelos Maratthon ili
kuitangaza vyema Tanznaia” alibainisha Frances.
Katika makubaliano hayo, Ngowi na Frances pia wataanzisha
mbio za “King Solomon Marathon” zitakazofanyika katika jiji la Addis Ababa
nchini Ethiopia.
Deidee Lorenz amefungua pazia kwa watu mashuhuri kushiriki
katika mbio za marathon nchini Tanzania na ni jukumu la Watanzania kuchangamkia
fursa zinazoletwa na ujio wao.
0 comments:
Post a Comment