Nguza kulia akiwa na mwanawe, Papii |
MWANAMUZIKI nguli wa dansi nchini, Nguza Viking amesema
kutoka gereza la Ukonga kwamba, hajagusa hata senti moja kutokana na mauzo ya
wimbo wake Seya na hajui fedha zilienda wapi.
Nguza ambaye gerezani anatumikia kifungo pamoja na wanawe
akikwemo Papii Kocha aliyerekodi naye wimbo huo kwa mara ya pili, jana alitembelewa
gerezani na mwanamuziki mwenzake, John Kitime.
Kitime aliporejea kutoka Gerezani, akaandika kwenye blog
yake; “Nimekwenda gereza la Ukonga asubuhi hii (jana) kumsalimia Nguza na
mwanae Papii, nimewakuta wachangamfu wenye afya nzuri. Nguza kanituma
NIWASALIMIE WOTE, naomba nitumie jukwaa hili kutangaza salamu hizo,”.
Nguza enzi za ujana wake |
“Ni wazi italazimika kuomba muda wa ziada kutoka kwa uongozi
wa Magereza kuzungumza zaidi na Nguza, jambo mojawapo ambalo tutalizungumza ni
kuhusu mapato ya wimbo wa Seya. Pamoja na umaarufu wote ni jambo la kusikitisha
kuwa Nguza anasema hajapata fedha yoyote kutoka wimbo ule, zaidi ya fedha
alizopewa kuingia studio kuurekodi. Swali ni nani anazipokea fedha za wimbo
ule?”ameandika Kitime.
Hii itakuwa kashfa nyingine kubwa kwa wadau wakubwa wa muziki
Tanzania, kwani wimbo huo ulikuwa katika mradi ulioandaliwa na jamaa mmoja
maarufu sana katika medani ya sanaa na burudani, anayeaminika hadi Ikulu,
uliotwa Baba na Mwana.
BIN ZUBEIRY haitaki kujikita sana kwenye suala hilo, ila
inakaribisha mjadala tena mpana tu, labda njia itapatikana.
Nguza wanawe, walihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa
makosa kumi ya kubaka watoto wenye umri kati ya miaka sita na minane na makosa
mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri huo huo kati ya Aprili na
Oktoba mwaka 2003 maeneo ya Sinza mjini Dar es Salaam.
Mwishoni mwa mwaka 2009, Babu Seya na wanawe Papii Nguza
'Papii Kocha, Nguza Mbangu na Francis Nguza walikata rufaa dhidi ya hukumu ya
kifungo cha maisha jela iliyotolewa na aliyekuwa Hakimu wa Mahakama ya Kisutu,
Addy Lyamuya, lakini akaachiwa mtoto wake mmoja tu, Francis ‘Chichi’.
0 comments:
Post a Comment