Ngassa mazoezini Azam FC |
Na Prince Akbar
WACHEZAJI wa Azam FC waliokuwa na timu ya taifa ya Tanzania,
Taifa Stars akiwemo Mrisho Khalfan Ngassa anayevumishiwa kuwa katika mpango wa
kurejea klabu ya zamani, Yanga leo wameanza mazoezi rasmi na timu hiyo, kwa
maandalizi ya klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Kutoka Azam, BIN ZUBEIRY imeelezwa kwamba, wachezaji
wanne hawakufanya mazoezi leo asubuhi, kwa sababu ambazo hazikuweza kufahamika
mara moja, hao ni makipa Deo Munishi ‘Dida’ na Mwadini Ally na viungo Waziri
Salum na Jabir Aziz na mshambuliaji John Bocco ‘Adebayor’.
Waziri aliripoti kambini wiki iliyopita na kutoa taarifa ya
kuuguliwa na baba yake akarejea Zanzibar na Stima alikuwepo tangu mazoezi
yanaanza, wakati Bocco alikuwa Taifa Stars.
Wachezaji wengine waliokuwa na timu ya taifa ya Zanzibar,
Zanzibar Heroes kwenye michunao ya Kombe la Dunia ya nchi zisizo wanachama wa
FIFA, Abdi Kassim ‘Babbi’, Abdulhalim Humud ‘Gaucho’, Abdulghani Gullam na
Hamisi Mcha tayari wameripoti na wameendelea na mazoezi leo Chamazi.
Kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.’ aliyeumia kabla ya
Stars kwenda Msumbiji, yeye anaendelea na programu maalum ya daktari wa timu
hiyo na tayari ameripoti.
John Bocco 'Adenayor' |
Tayari Azam, washindi wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara wamekwishamalisha usajili wa wachezaji wao hata kabla ya kwenda
likizo.
Programu ya maandalizi ya Kombe la Kagame, inayoendelea hivi
sasa itamalizika siku moja kabla ya kuanza mashindano hayo, Juni 28 na
yatakapomalizika, wachezaji watapewa mapumziko ya siku chache kabla ya kuanza
maandalizi kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu.
Maandalizi kwa ajili ya VPL yatahusisha pia ziara ya nje ya
nchi ya kujiandaa na msimu mpya, ingawa amesema nchi hiyo itatajwa baadaye.
Wachezaji wapya kikosini Azam msimu huu ni kiungo Mkenya
George ‘Blackberry’ Odhiambo na kipa Deogratius Munishi kutoka Mtibwa Sugar,
wakati Aishi Salum, Jackson Wandwi, Dizana, Ibrahim Rajab Jeba na Joseph
Kimwaga, wamepandishwa kutoka akademi ya Azam.
Kikosi kamili cha Azam FC kinaundwa; na makipa, Mwadini
Ally, Deo Munishi ‘Dida’ Aishi Salum na Jackson Wandwi, mabeki wa Ibrahim
Shikanda, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Samir Haji Nuhu, Luckson Kakolaki, Said
Mourad, Joseph Owino na Aggrey Morris.
Viongo ni Kipre Bolou, Abdulhalim Humud, Himid Mao, Salum
Abubakar, Abdi Kassim Sadalla, Ramadhani Suleiman Chombo, Abdulghani Ghullam,
Ibrahim Rajab Jeba, Jabir Aziz Stima, Ibrahim Joel Mwaipopo, Kipre Tchetche,
Mrisho Ngassa, Zahoro Pazi, Khamis Mcha na George Odhiambo ‘Blackberry’ wakati
washambuliaji ni Gaudence Mwaikimba, John Bocco ‘Adebayor’.
Hii ni mara ya kwanza kwa Azam FC kucheza Kombe la Kagame, baada
ya kushika nafasi ya pili katika msimu uliopita wa Ligi Kuu. Katika Kombe la
Kagame mwaka huu, wenyeji Bara wataingiza timu tatu, Yanga ambao ni mabingwa
watetezi, wakati Simba na Azam wanaingia kwa nafasi za uwakilishi.
0 comments:
Post a Comment