Tetesi za J'tatu magazeti Ulaya
M'VILLA AICHAGUA ARSENAL
KIUNGO wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Rennes, Yann M'Vila, 21, amesema kwamba anapenda kujiunga na Arsenal wakati, kocha wa The Gunners, Arsene Wenger anatazamiwa kukamilisha biashara hiyo mapema tu katika dirisha la usajili.
KIUNGO Luka Modric yupo karibu kuhamia Hispania, na Real Madrid iko tayari kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 wa Tottenham.
KLABU ya Barcelona ina mpango wa kumsajili mchezaji mwenzake, kiungo Luca Modric katika klabu na timu ya taifa, beki Vedran Corluka mwenye umri wa miaka 26.
KLABU ya West Ham ina mpango wa kumsajili mshambuliaji Joselu, mwenye umri wa miaka 22 wa Real Madrid, ambaye kocha wa Arsenal, Arsene Wenger anamtolea macho pia.
KLABU ya Liverpool ina mpango wa kumsajili beki wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Schalke, Benedikt Howedes, mwenye umri wa miaka 24, na inandaa ofa wakati kocha Brendan Rodgers akiwa katika mpango wa kuimarisha safu yake ya ulinzi.
WAKALA wa beki wa Ajax, Jan Vertonghen, mwenye umri wa miaka 25, amesema kwamba mpango wa mteja wake kwenda Tottenham unaendelea licha ya kufukuzwa kwa kocha Harry Redknapp.
KLABU ya Swansea inataka kumsajili mshambuliaji wa Sweden, Markus Rosenberg, mwenye umri wa miaka 29, ambaye yuko huru baada ya kuitumikia kwa miaka mitano Werder Bremen.
TETESI ZA EURO 2012
BEKI wa zamani wa England, Alvin Martin haamini kama timu hiyo itatinga Robo Fainali, akisema kwamba wanahitaji zaidi bahati kufanikiwa katika hilo.
KOCHA wa Jamhuri ya Ireland, Giovanni Trapattoni amepigwa zengwe lingine baada ya Nahodha wa zamani wa timu hiyo, Roy Keane kutoa taarifa ya kumkandia tena.
LIVERPOOL WABEBA KINDA LA MAN CITY
KOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers analitaka kinda la Manchester City, Barry Hunter katika mpango wake wa kutengeneza mradi baaab kubwa wa soka ya vijana Anfield.
0 comments:
Post a Comment