Kikosi cha Simba kilicho ziarani Kanda ya Ziwa |
Na Princess Asia
BAADA ya jana kuichapa Toto African ya Mwanza mabao 2-0 katika mechi kali ya kirafiki iliyofanyika Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, mabingwa wa Tanzania, Simba SC leo wanashuka tena dimbani kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga kumenyana na mabingwa wa Uganda, Express ‘Tai Mwekundu’.
BAADA ya jana kuichapa Toto African ya Mwanza mabao 2-0 katika mechi kali ya kirafiki iliyofanyika Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza, mabingwa wa Tanzania, Simba SC leo wanashuka tena dimbani kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga kumenyana na mabingwa wa Uganda, Express ‘Tai Mwekundu’.
Ofisa
Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga ‘Mr Liverpool’ ameiambia BIN ZUBEIRY leo asubuhi
kwamba tayari wako njiani kuelekea Shinyanga baada ya mechi ya jana.
Katika
mchezo wa jana Mwanza, Wekundu wa Msimbazi walianza pambano hilo kwa kasi na
iliwachukua dakika 17 tu kuandika bao la kwanza lililowekwa kimiani na Uhuru
Selemani aliyemalizia vizuri pasi ya Abdallah Juma.
Hadi
kipindi cha kwanza kinamalizika, Simba ilikuwa inaongoza kwa bao hilo moja.
Katika
kipindi cha pili, Simba ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Abdallah Seseme na
Hassan Khatib na nafasi zao kuchukuliwa na William Lucian (Gallas) na Jonas
Mkude.
Mabadiliko
hayo yalizaa matunda kwani katika dakika ya 48, Simba iliandika bao la pili
lililofungwa na Salim Kinje, mchezaji mpya wa Simba aliyesajiliwa kutoka AFC
Leopards ya Kenya.
Kinje
alifunga bao hilo akiunganisha moja kwa moja kutoka nje ya 18 pasi ya kichwa
kutoka kwa Uhuru.
Katika
pambano la jana, wachezaji waliosajiliwa msimu huu walikuwa ni Waziri Hamad,
Paulo Ngalema, Kiggi Makassy, Kinje na
Abdallah Juma.
Wachezaji
wawili wa kikosi cha vijana Simba maarufu kwa jina la U-20, Haruna Chanonga na
Lucian pia walicheza mechi yao ya kwanza kwa kikosi cha wakubwa leo hii.
Juni
24 Simba itaingia kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga kupambana na mabingwa wa
soka wa Uganda, Express FC.
SIMBA;
Waziri, Hassan (Gallas), Ngalema (Omar Waziri), Obadia Mungusa, Haruna Shamte,
Amri Kiemba (Edward Christopher), Chanonga, Seseme (Kiggi), Abdallah (Ramadhani
Salum), Kinje na Uhuru.
Wakati huo huo: Kocha Mkuu wa Simba, Mserbia Milovan Cirkovic anatarajiwa kutua wakati wowote kuanzia sasa kutoka nyumbani, Serbia alikokuwa kwa mapumziko.
0 comments:
Post a Comment