Mkwasa |
KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya wanawake Tanzania, Twiga
Stars, Charles Boniface Mkwasa amejiuzulu leo.
Nahodha huyo wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania,
Taifa Stars ameiambia BIN ZUBEIRY usiku huu kwamba ameamua
kujiuzulu kutokana na matokeo mabaya na pia timu hiyo kutothaminiwa na
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Mkwasa anachukua hatua hiyo, siku mbili tu tangu timu hiyo
itolewe katika kinyang’anyiro cha kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la
Mataifa ya Afrika na Ethiopia kwa jumla ya mabao 3-1, ikifungwa 2-1 Addis Ababa
na baadaye 1-0 Jumamosi mjini Dar es Salaam.
Mapema baada ya kufungwa juzi, Mkwasa alisema kwamba timu
hiyo haikuwa na maandalizi mazuri na TFF haikuonekana kuijali kabisa. Lakini Mkwasa
atakumbukwa mno kwa kuifikisha juu timu hiyo, akiiwezesha kushiriki fainali za
Afrika miaka miwili iliyopita nchini Afrika Kusini, hiyo ikiwa ni mara ya
kwanza kihistoria.
0 comments:
Post a Comment