David Beckham anaongoza kwa wanasoka, Ronaldo ampiku Messi

BONDIA Floyd Mayweather amempiku Tiger Woods katika orodha ya wanamichezo matajiri duniani kwa mujibu 100 bora iliyotolewa na jarida la Forbes kwa wanamichezo walioingiza fedha nyingi mwaka jana.
Bondia Mayweather, kwa sasa anatumikia kifungo cha miezi mitatu jela kwa unyanyasaji, almeingiza pauni Milioni 54.25, kiwango ambacho kimeongezeka kutokana na kupromoti mwenyewe mapambano yake.
Gwiji wa Gofu, Woods ameshuka hadi nafasi akiwa ameingiza pauni Milioni 37.92 na Manny Pacquiao amepanda nafasi ya pili kwa kuingiza Pauni Milioni 39.57.
David Beckham anashika nafasi ya nane kwenye orodha hiyo.
Ni mwanasoka anayeongoza kwa kulipwa, akiwa ameingiza pauni Milioni 29.36.

WANAMICHEZO 10 MATAJIRI DUNIANI:

Floyd Mayweather $85m (£54.25m)
Manny Pacquiao $62m (£39.57m)
Tiger Woods $59.4m (£37.92m)
LeBron James $53m (£33.84m)
Roger Federer $52.7m (£33.64)
Kobe Bryant $52.3m (£33.38m)
Phil Mickelson $47.8m (£30.51m)
David Beckham $46m (£29.36m)
Cristiano Ronaldo $42.5m (£27.10m)
10 Peyton Manning $42.4m (£27.06m)
Ajabu, bingwa wa Riadha wa Olympiki mbio fupu na anayeshikilia rekodi ya dunia, Usain Bolt, ambaye ni nyota mwenye jina kubwa zaidi kuelekea Olimpiki ya London 2012, anashika nafasi ya 63, akiwa ameingiza Pauni Milioni 12.96, ambayo ni sawa na robo ya pato la Mayweather.
Pia anapata nusu ya anachopata mcheza gofu Phil Mickelson, pauni Milioni 30.51.
Woods aliongoza orodha ya Forbes tangu mwaka 2001, lakini anaonekana kushuka kwa pauni Milioni 10.21 kutoka mwaka uliotangulia ambao pia alishuka kwa kiasi cha nusu kutoka pato lake la mwaka 2009.
Amekuwa katika wakati mgumu tangu akumbwe na kashfa ya ngono.
Nyota wa Miami Heat, LeBron James anashika nafasi ya nne akiwa ameingiza Pauni Milioni 33.84 akiwa anaongoza katika wacheza kikapu 13 waliomo kwenye orodha hiyo. Mcheza tenisi wa Uswisi, Roger Federer ni wa tano kwa kuingiza Pauni Milioni 33.64.
Nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameingiza Pauni Milioni 27.10 na imetokana na mshahara mkubwa anaoupata kuliko mchezaji yeyote katika ligi yeyote, pauni Milioni 12.75.
Wanawake wawili tu wameingia katika orodha hiyo, mcheza tenisi wa Urusi, Maria Sharapova katika nafasi ya 26, pauni Milioni 17.79.
Bingwa wa michuano ya Mchina bingwa wa French Open mwaka jana, Li Na ni wa 81 akiwa ameingiza pauni Milioni 11.72, baada ya kuibuka mzaliwa wa kwanza wa bara la Asian kutwaa taji la Grand Slam kwa mchezaji mmoja mmoja.